Simba, Yanga kuanza hivii

Saturday September 25 2021
MECHI PIC
By Ramadhan Elias

TAYARI vikosi vya Simba na Yanga vitakavyoanza kwenye mechi ya Ngao ya Hisani leo saa 11:00 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa vimewekwa wazi.

Simba ambao ni wenyeji wameanza na kipa, Aishi Manula na mabeki wanne Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Joash Onyango na Pascal Wawa.

Viungo ni Thadeo Lwanga, Sadio kanoute, Pape Sakho, Rally Bwalya na Hassan Dilunga huku Chris Mugalu akisimama eneo la mshambuliaji mmoja.

Benchi la Simba wapo, Beno Kakolanya, Gadiel Michael, Israel Mwenda, Peter Banda, Erasto Nyoni, Mzamiru Yassin, John Bocco, Kennedy Juma na Yusuph Mhilu.

Yanga imeanza na kipa, Djigui Diarra na mabeki Djuma Shaban, Kibwana Shomary, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto.

Viungo ni Khalid Aucho, Yannick Bangala, na Feisal Salum huku mbele wakisimama Fiston Mayele, Moloko Jesus na Farid Mussa.

Advertisement

Benchi wapo Deus Kaseke, Ramadhan Kabwili, Abdallah Haji, Zawadi Mauya, David Bryson, Ditram Nchimbi, Yacouba Songne, Heritier Makambo na Yusuph Athuman.

Advertisement