Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama la Wana lina dakika 90 Tanzanite Kwaraa

STAND Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, mjini Babati, mkoani Manyara, ni ya marudiano baada ya ile ya kwanza iliyopigwa CCM Kambarage mjini Shinyanga Julai 4, 2025, Stand inayoshiriki Ligi ya Championship kuchapwa mabao 3-1.

Stand United ‘Chama la Wana’, ina dakika 90 ngumu za kupindua meza, itakapokuwa ugenini leo Jumanne katika mechi ya marudiano ya ‘Play-Off’ kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao dhidi ya Fountain Gate.

Mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, mjini Babati, mkoani Manyara, ni ya marudiano baada ya ile ya kwanza iliyopigwa CCM Kambarage mjini Shinyanga Julai 4, 2025, Stand inayoshiriki Ligi ya Championship kuchapwa mabao 3-1.

Kwa maana hiyo, Stand inahitaji kushinda mabao 3-0, leo ili kupanda Ligi Kuu Bara baada ya kushuka daraja msimu wa 2018-2019 na kutoka Championship iliyoshiriki msimu wa 2024-2025 na kumaliza nafasi ya tatu na pointi 61.

Kwa upande wa Fountain, kina faida zaidi tofauti na wapinzani wao kutokana na ushindi wa mabao 3-1, mechi ya kwanza, hivyo kusubiriwa kuona kama Stand itapindua meza na kupanda Ligi Kuu Bara au itabakia Championship msimu ujao.

Stand iliyomaliza nafasi ya tatu na pointi 61, imefikia hatua hiyo baada ya kuiondoka Geita Gold iliyomaliza ikiwa ya nne na pointi 56, katika mechi pia ya mtoano kwa jumla ya mabao 4-2.

Kwa upande wa Fountain, ilimaliza nafasi ya 14 na pointi 29 katika Ligi Kuu msimu wa 2024-2025 na kukutana na Tanzania Prisons iliyomaliza ya 13 na pointi 31, kwenye mechi ya mtoano na kikosi hicho cha maafande kushinda jumla ya mabao 4-2.

Katika mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Fountain ilitoka sare ya bao 1-1, Juni 26, 2025, kisha marudiano Juni 30, 2025, ikachapwa mabao 3-1 na maafande kubakia Ligi Kuu msimu ujao.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha wa Fountain, Mohamed Ismail ‘Laizer’, alisema licha ya ushindi wa mechi ya kwanza, ila amewataka wachezaji wa kikosi hicho kupambana na kutobweteka, kutokana na kutojua wapinzani wao wataingia na mbinu gani.

Kwa upande wa Kocha wa Stand United, Juma Masoud, alisema kiungo wa timu hiyo, Yusuph Khamis aliyeanguka uwanjani ghafla mechi ya kwanza ataangalia kama atakuwa fiti, japo kwa sasa hali yake imeimarika baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini. “Tulifanya makosa binafsi yaliyotugharimu mechi ya kwanza, lakini tumeyafanyia kazi kwa muda mchache uliopo, tunahitaji kuongeza umakini na utulivu mkubwa ili kutimiza malengo yetu, sio rahisi kwetu japo hatujakata tamaa,” alisema Masoud.