Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yamtisha beki wa Wydad

Muktasari:

  • Beki huyo ameliambia Mwanaspoti kwa simu kuwa mchezo dhidi ya Simba siyo rahisi kutokana na mabadiliko ya kikosi cha wekundu hao.

WAKATI klabu ya Simba ikiendelea na maandalizi kabla ya kuivaa Wydad Casablanca kesho jijini Marrakech, Morocco huku beki wa timu hiyo ya Afrika Kaskani, Arsene Zolla akionekana kuingiwa ubaridi kwa kuihofia Simba.

Beki huyo ameliambia Mwanaspoti kwa simu kuwa mchezo dhidi ya Simba siyo rahisi kutokana na mabadiliko ya kikosi cha wekundu hao.

Zolla alisema, Simba sio timu rahisi kutokana na wachezaji walionao kwenye kikosi chao ambao wengi ni wale wenye uzoefu mkubwa na mashindano kama hayo ya Ligi ya Mabingwa

Beki huyo amemuelezea kiungo Fabrice Ngoma kama ingizo muhimu ndani ya Simba na kwamba Mkongomani huyo ni mchezaji anayejua vyema soka la Wydad baada ya kuichezea Raja Athletic.

“Unakumbuka tulivyocheza nao huku mara ya mwisho walionyesha mchezo mkubwa lazima unapokwenda kukutana na timu kama hiyo mnatakiwa kuwa makini,” alisema Zolla.

“Wana wachezaji waliokomaa sana na mashindano kama haya na unaona sasa wamemuongeza ndugu yangu  Fabrice (Ngoma) ni mchezaji mkubwa tunamjua na anaijua Wydad utaona kwamba timu yao sio mbaya.

Aidha Zolla aliongeza hatua ya kikosi cha Wydad kushinda mabao 3-1 jana mechi ya Ligi Kuu mbele ya Mouloudia Oujda, ni hatua nzuri ya kujiandaa na mchezo huo wa kesho wakiwa na morali.

“Tulikuwa hatujashinda mechi nne mfululizo, lakini sasa angalau tumepata nguvu kuikabili Simba.”