Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yamtambulisha Kanoute

MABINGWA wa Ligi Kuu Bara wamefunga usajili wa msimu huu baada ya kumalizana na kiungo kutokea Mali, Sadio Kanoute ambaye awali Mwanaspoti lilikujuza ujio wake wa kukamilisha dili hilo.

Kanoute anakuwa mchezaji wa kumi katika kikosi hicho kusajiliwa lakini anakuwa na wanne kutambulishwa huku wakibakia Kibu Denis na Jeremia Kisubi ambao walishindwa kusafiri na kikosi hicho kwenda Morocco.

Baada ya kutambulishwa kama mchezaji mpya wa Simba Kanoute alisema kwa ufupi "Ni mchezaji mpya wa klabu hii," kuongezea;

"Kanoute alisema anawahidi mashabiki wa Simba amekuja kucheza mechi nyingi za timu hiyo na kuhakikisha anatoa mchango wake kwa ajili ya kupata mataji."

Mwanaspoti linafahamu usajili huo ni mapendekezo ya kwanza kocha, Didier Gomes ambaye katika ripoti yake alihitaji kiungo mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya ukabaji na kushambulia.

Kanoute kusajiliwa kwake anakwenda kuongeza ushindani wa nafasi ya kucheza katika nafasi ya kiungo wa kati dhidi ya Taddeo Lwanga ambaye alicheza zaidi msimu uliopita pamoja na Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Erasto Nyoni na Abdulsamad Kassim aliyesajiliwa msimu huu akitokea Kagera Sugar.

Katika hatua nyingine Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema benchi la ufundi wamemua kucheza mechi za kirafiki ili kuona mambo matatu makuu yamefanyiwa kazi.

Rweyemamu alisema jambo la kwanza katika mazoezi yao kuna vitu vya kufundi pamoja na utimamu wa mwili ambavyo benchi la ufundi liliwapatia wachezaji kwa maana hiyo katika mechi hizo za kirafiki wanataka kuviona.

Alisema kama wakiviona vitu hivyo vya kiufundi katika michezo yao ya kirafiki maana yake wachezaji watakuwa wameyafanyia kazi kama ambavyo walikuwa wanahitaji kuviona kutoka kwao.

"Taarifa za kuhusu kama kutakuwa na mashindano ya ambayo tutakutana na watani zetu Yanga ambao nao wapo huku kambini kwa ajili ya maandalizi hilo wala hatulifahamu."