Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yampigia hesabu kipa Berkane

KIPA Pict

Muktasari:

  • RS Berkane imechukua ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika mara mbili tofauti na Simba haijawahi kutwaa ubingwa wa mashindano ya klabu Afrika.

Kocha wa Simba, Fadlu Davids amesema wamejipanga kikamilifu kuikabili RS Berkane katika mechi ya kwanza ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu, kesho Jumamosi.

Davids amesema kuwa wameifanyia Berkane tathmini ya kina kama timu na kwa wachezaji wake - mmoja mmoja.

Katika tathmini hiyo ya wachezaji mmoja mmoja wa Berkane, Simba imeamua kushughulika zaidi na kipa namba moja wa timu hiyo, Mohammed Munir.

Fadlu amesema kuwa wanapaswa kutumia akili kubwa kumdhibiti Munir kwa vile ndio anabeba ushindi wa RS Berkane.


“Ni muhimu kwetu kuzitawala nafasi kwa mchezo. Tunaufahamu huu uwanja na kocha wao hivyo ni muhimu sana kwa wachezaji kuelekeza akili kwenye mchezo tu. 

“Kipa wao (Munir) amekuwa mchezaji muhimu kwenye timu tangu aliposajiliwa. Tunatakiwa kucheza mechi hii kama michezo mingine. Hatutakiwi kufikiria nyakati kadhaa tu maana sio rahisi kukabiliana RS Berkane kwa staili hiyo,” amesema Davids.

Munir ndio kipa anayeongoza kwa kucheza idadi kubwa ya mechi kwenye mashindano hayo bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa (clean sheets) ambapo amefanya hivyo katika michezo nane.

Kipa huyo anaongoza pia kwa kuwa na wastani mzuri wa kuokoa hatari kwenye mashindano hayo akiwa na wastani wa kufanya hivyo akiwa na asilimia 84.6 na hadi sasa ameruhusu nyavu zake kutikiswa Mara mbili tu.

Davids pia amesema anamfahamu vyema kocha wa Berkane, Moine Chabaan kwa vile amewahi kukutana naye mara kadhaa.

“Kocha wa Berkane amefanya kazi kubwa tangu alipojiunga nayo kutokea Raja. Ni timu yenye uwezo kimbinu wa kuukabili mchezo na jambo la muhimu kwetu ni namna gani ya kupunguza makali yao.

“Uwanja wao una eneo zuri la kuchezea. Tunajua watakuja na kasi na nguvu kubwa katika dakika 45 za kwanza. Msimu huu timu yangu imeonyesha utayari wa kucheza katika viwanja vyenye ubora tofauti wa eneo la kuchezea,” amesema Davids.