Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yalamba dili la Sh4 bilioni

Muktasari:

  • Mkataba huo umesainiwa jana jijini Dar es Salaam baada ya klabu hiyo kumalizana na Kampuni ya Vunja Bei iliyoingia nao miaka miwili iliyopita ukiwa na thamani ya Sh 2 Bilioni.

KLABU ya Simba imelamba dili nono ya Sh 4 Bilioni baada ya kuingia mkataba mpya wa miaka miwili wa makubaliano ya kutengeneza na kusambaza jezi na Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited.

Mkataba huo umesainiwa jana jijini Dar es Salaam baada ya klabu hiyo kumalizana na Kampuni ya Vunja Bei iliyoingia nao miaka miwili iliyopita ukiwa na thamani ya Sh 2 Bilioni.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Ahmed Ally, aliliambia Mwanaspoti jana kuwa, wameamua kuingia mkataba na Sandaland baada ya kuvutiwa na ofa yao iliyokuwa mara mbili na ile iliyopita ya Vunja Bei.

"Tunajivunia kwa kupata mkataba huu ambao utakuwa ni wa kutengeneza na kusambaza jezi za timu zetu. Ilikuwa ngumu kukataa ofa hii ya Sandaland na utakuwa wa miaka miwili na kila msimu itakuwa ni Sh 2 Bilioni, ikiwa na maana kwa miaka miwili klabu inavuna Sh 4 Bilioni," alisema Ally.

Awali Mwanaspoti lilidokezwa, Sandaland, ni moja ya kampuni ya Watanzania inayohusika na kuuza jezi ndani na nje ya nchi waliokuwa sehemu ya walioonda tenda, kampuni nyingine zikiwa ni Puma ya Afrika Kusini  ambao nao walitoa ofa yao, lakini mabosi wa Simba wakavutiwa na kampuni hiyo.

Kulingana na mkataba huo, Sandaland wamepewa haki ya kuisimamia Simba kwenye matukio yake ya kimichezo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mashabiki kununua jezi na kwenda uwanjani na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Yusuf Omar Yenga aliwaahidi wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba kuwa watashuhudia jezi zenye ubora na zitakazopatikana kwa haraka kwani kwa sasa mzigo upo njiani unakuja.

"Tunawaahidi mashabiki kupata jezi zenye ubora na zitakazopatikana kwa wakati kabla hata ya Tamasha ya Simba Day, kwa vile mzigo kwa sasa upo njiani na tumejipanga kuusambaza mapema na kumfikia kila Mwanasimba," alisema Yenga aliyefafanua wameanza kupokea oda za mawakala mikoani ili mzigo ukija usambazwe kuwawezesha wanasimba kupata jezi kirahisi popote alipo.

Yenga alisema Sandaland ina maduka makubwa mawili ya kuuza jezi jijini Dar es Salaam ambayo itawarahisisha wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba kupata jezi za msimu ujao kirahisi, huku wale wa mikoani watapata kwa mawakala watakaojiorodhesha na kuweka oda zao kuanzia sasa.