Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Azam FC wapewa wiki tatu

MASTAA Pict

Muktasari:

  • Azam iliyoshindwa kufikia malengo yake msimu huu baada ya kukosa mataji yote imemaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo na imejihakikishia kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

KIKOSI cha Azam FC kimepewa mapumziko ya wiki tatu kabla ya kurejea wiki ya nne tayari kwa ajili ya kujiweka sawa kwa msimu mpya 2025/26.

Azam iliyoshindwa kufikia malengo yake msimu huu baada ya kukosa mataji yote imemaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo na imejihakikishia kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Azam, kimeliambia Mwanaspoti kuwa wametoa wiki tatu za mapumziko baada ya hapo timu itarejea haraka kambini kwaajili ya kupokea mipango mipya chini ya benchi jipya.

Mwanaspoti linafahamu na lilisharipoti kuwa kocha Florent Ibenge ndiye atakayekuwa kocha mkuu wa timu hiyo hivyo mipango ni kukutana na kikosi kabla ya kwenda mafichoni kujiwinda na msimu mpya.

“Wiki moja timu itakuwa na maandalizi jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda sehemu ambayo mwalimu ataipendekeza. Kuhusu usajili mchakato unaendelea na tayari tumeshasajili baadhi ya wachezaji,” alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza;

“Mipango na mikakati ipo chini ya kocha. Hadi muda huu hatufahamu kambi itawekwa wapi, ila nafikiri wiki ya nne ambayo atakutana na wachezaji kila kitu kitawekwa wazi.”