Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaitangulia Yanga Kwa Mkapa

ZIMEWASILI Pict
ZIMEWASILI Pict

Muktasari:

  • Msafara wa Simba umefika uwanjani hapo saa 9:26 alasiri ikiwa kwenye basi lao kubwa, huku mbele kukiwa na ya askari polisi.

KIKOSI cha Simba kimekuwa cha kwanza kuwasili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ikiwatangulia wenyeji, Yanga kwa dakika mbili na kuliamsha shangwe kwa mashabiki wa timu hizo walianza kuujaza uwanja huo.

Msafara wa Simba umefika uwanjani hapo saa 9:26 alasiri ikiwa kwenye basi lao kubwa, huku mbele kukiwa na ya askari polisi.

Wakati Simba ikifika uwanjani hapo na mashabiki wachache wa timu hiyo, walilipuka kwa shangwe wakipata uhakika wa timu yao kucheza mechi hiyo.

Sio Simba pekee hata mashabiki wa Yanga nao waliishangilia kuwaona watani wao wakiwasili uwanjani hapo.

Hata hivyo, Simba ilipoingia tu Yanga nao ilifuata dakika mbili baadaye yaani saa 9:28 alasiri wakiwa kwenye mabasi mawili madogo aina ya coaster nyeupe.

Nyuma ya basi hilo ilipofika saa 9:35, Yanga ikaingiza basi lao maalum la wachezaji likiwa halina mtu yeyote likisindikizwa na pikipiki ya king'ora n kuufanya uwanja kulipuka kwa shangwe za mashabiki ambao wameonekena kuwa na mzuka kwa mechi hiyo ya kiporo cha Dabi ya Karikoo ya Ligi Kuu.

Mechi hiyo ikliyoahirishwa mara mbili Machi 8 na Juni 15 inapigwa kuanza saa 11:00 jioni ya leo, huku Yanga ikiwa wenyeji na wanaoongoza msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 79 dhidi ya 78 za Simba inayoshika nafasi ya pili na kila moja inapiga hesabu za ubingwa baada ya dakika 90.

Yanga inahitaji sare yoyote au ushindi kutangaza ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo, wakati Simba yenyewe inahitajika kushinda ili kulirejesha taji hilo la Ligi Kuu iliyolitema misimu mitatu mfululizo kwa watani hao wao wanaoshikilia rekodi ya kulitwaa mara 30, nane zaidi na iliyonayo Wekundu hao.