Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaipiga bao tena Yanga

BAO Pict

Muktasari:

  • Simba ililazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na RS Berkane ya Morocco baada ya awali kupoteza ugenini kwa mabao 2-0 katika mechi za fainali za michuano hiyo, lakini licha ya kulikosa taji hilo lililokuwa limetemwa mapema na waliokuwa watetezi, Zamalek ya Misri, ila kuna kitu imewapiga bao Yanga.

HUKO mtaani mashabiki wa Yanga wanaendelea kuchekea tumboni baada ya watani wao, Simba kushindwa kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu tofauti na ile kauli mbiu yao ya 'Hii Tunabeba'.

Simba ililazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na RS Berkane ya Morocco baada ya awali kupoteza ugenini kwa mabao 2-0 katika mechi za fainali za michuano hiyo, lakini licha ya kulikosa taji hilo lililokuwa limetemwa mapema na waliokuwa watetezi, Zamalek ya Misri, ila kuna kitu imewapiga bao Yanga.

Ndio, kitendo cha Simba kufika hadi fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu na kukosa taji mbele ya RS Berkane ya Morocco, kimeifanya timu hiyo kufikisha pointi 48, ikishika nafasi ya tano kwa viwango vya ubora barani Africa (CAF), huku Yanga ikiwa ya 11.

Simba iliyofika hadi fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu baada ya kusota kwa miaka 32, tangu mara ya mwisho ilipocheza mwaka 1993 na kulikosa, ilikosa tena ubingwa huo kwa kuchapwa jumla ya mabao 3-1, dhidi ya RS Berkane.

Viwango hivyo, ni kwa jumla ya miaka mitano ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika, ambapo kikosi hicho kimekusanya pointi hizo nyuma ya mabingwa wa kihistoria, Al Ahly ya Misri inayoongoza kwa kukusanya pointi 78.

Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini iliyokosa pia taji la Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu baada ya kuchapwa na Pyramids FC ya Misri kwa jumla ya mabao 3-2, inashika nafasi ya pili na pointi 62, ikifuatiwa na ES Tunis ya Tunisia yenye 57.

Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, RS Berkane inashika nafasi ya nne na pointi 52, ikifuatiwa na Simba yenye 48, huku Pyramids FC  ambao ni Mabingwa Ligi ya Mabingwa Afrika ni ya sita na 47, Zamalek ya Misri ina pointi 42, wakati Wydad Casablanca ya Morocco ni ya nane na 39.

USM Alger ya Algeria inashika nafasi ya tisa na pointi 37, huku CR Belouizdad ya Algeria iko nafasi ya 10 na pointi 36, Yanga iliyofika fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu wa 2022-2023, inashika nafasi ya 11 na pointi 34.

Yanga ilifika hadi fainali hiyo na kukosa ubingwa huo mbele ya USM Alger ya Algeria kwa faida ya bao la ugenini, baada ya kuchapwa jijini Dar es Salaam mabao 2-1, Mei 28, 2023, kisha marudiano kushinda bao 1-0, mechi ikipigwa Juni 3, 2023.

1. Al Ahly pointi    -78

2.Mamelodi pointi -62

3.ES Tunis pointi -57

4.RS Berkane pointi- 52

5.Simba  pointi  -48

6.Pyramids pointi-47

7.Zamalek SC pointi-42

8.Wydad Casablanca pointi-39

9.USM Alger pointi -37

10.CR Belouizdad pointi -36

11.Yanga pointi -34