Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaichapa Ndanda…kituo kinachofuata…

Muktasari:

Simba imefikisha pointi 34 kileleni baada ya kucheza mechi 13 ikifuatiwa na Yanga (24) kabla ya mechi baina yao itakayochezwa Jumamosi ya Januari 4, 2020

Dar es Salaam. Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wametuma salamu zao kwa Yanga baada ya kuichapa Ndanda FC kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Vinara hao wa Ligi Kuu, Simba ilipata mabao yake mawili yaliyofungwa na Francis Kahata pamoja na Deo Kanda aliyepewa bao la pili, lakini picha za marudio televisheni zilionyesha mpira hakuugusa mpira uliopigwa na beki Gadiel Michael kabla ya kuingia golini.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 34 kileleni baada ya kucheza mechi 13 ikifuatiwa na Yanga (24) hivyo kufanya mechi baina yao itakayochezwa Jumamosi ya Januari 4, 2020 kuwa na utamu wa aina yake.

Simba chini ya kocha Sven Vandenbroeck imeshinda mechi zake nne za mashindano yote na jambo linalowake katika mazingira mazuri ya kuingia kwa kujiamini katika mchezo wa Jumamosi.

Simba ilianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza katika dakika 13, lililofungwa na Francis Kahata kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja wavuni na kumwacha kipa wa Ndanda, Ally Mustapha asijue la kufanya.

Katika mchezo huo, kocha wa Simba, Sven alimwanzisha kwa mara ya kwanza, nahodha John Bocco na Hamisi Said 'Ndemla' pamoja na Erasto Nyoni ambao muda mrefu hawajaonekana uwanjani kwa sababu mbalimbali.

Simba ilionekana kucheza bila presha kutokana na maelewano mazuri yaliyopo baina ya viungo na washambuliaji na kufanya mabeki wao wasiwe na kazi ngumu ya kuhangaika huku kipa Aishi Manula akionekana kwenda likizo ya muda.

Hata hivyo kazi kubwa kwa Ndanda ilifanya na Kipa, Ally Mustafa 'Bathezi' ambaye alikuwa akifanya kazi ya ziada kuchomoa michomo iliyokuwa inaelekealangoni mwake akisaidiana vyema na beki zake, Said Shaban na Samwel John.

Mfumo walioutumia Ndanda FC wa kujilinda haukuwasaidia zaidi ya kumruhusu mashambukizi na kusababisha kuruhushu bao la pili lililofungwa na Deo Kanda dakika ya 86 na kuifanya Simba kuvuna ushindi huo na kujikita kileleni ikiwa na alama 34.

Katika mchezo mwingine Mwadui ililazimika kutoka nyuma na kulazimisha sare 1-1 na KMC katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja Mwadui Complex.

KMC ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia Abdul Hilal katika dakika 15, kabla ya Enock Mkanga kuisawazishia Mwadui katika dakika 71.

Vikosi

Simba: Aishi Manura, Haruna Shamte, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Kennedy Juma, Jonas Mkude/ Mzamiru Yassin, Ibrahim Ajibu/ Deo Kanda Sharaf Shibou b, Johy Bocco, Said Hamisi 'Ndemla' na Francis Kahata/ Deo Kanda.

Ndanda FC: Ally Mustafa, Shafii Naimu, Said Shaban, Samwel John, Paul Naona, Hemed Koja, Geofrey Joackim, Taro Joseph, Nassoro Salehe/ Omary Ramadhan, Kigi Makasi na Omary Hamisi.