Simba yaichapa Cosmo mabao 5-1

Klabu ya Simba ikiendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia Septemba 16 leo imecheza mechi ya kirafiki na kushinda mabao 5-1 dhidi ya Cosmopolitan.
⚽ Phiri - bao la kwanza amefunga Phiri kwa tikitaka dakika ya 14. Alifunga pia mechi ya kirafiki dhidi ya Kipanga kwenye ushindi wa mabao 3-0.
⚽ Baleke - amefunga bao la pili baada ya mabaki kushindwa kuokoa pasi ya Moses Phiri.
⚽ Onana - amefunga la tatu dakika ya 25 baada ha beki Mohammed Hussein kupiga krosi kisha Shomari Kapombe kumtengea Onana aliyeweka mpira wavuni
⚽ Kramo - aliingia dakika ya 57 na dakika ya 58 akimalizia kona iliyopigwa na Luis Miquissone.
⚽ Chilunda - dakika ya 85 alifunga bao akipiga shuti nje ya 18.
Bao la Cosmo limepatikana kwa mkwaju wa penalti baada ya beki Kapombe kuokoa mpira uliokuwa unaenda wavuni kwa mkono na kupewa kadi nyekundu.