Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaseja awaita nyota Kagera Sugar Dar

Muktasari:

  • Kagera iliyoshuka daraja ikishika nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu kwa sasa itakuwa wageni wa Namungo Juni 18 na Kaseja ameona hakuna sababu ya kwenda kukutana kambini mjini Bukoba na badala yake watajiandaa wakiwa Dar kwani watamalizia mechi na Simba Juni 22.

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Juma Kaseja amewaita wachezaji wa timu hiyo haraka kambini jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mechi mbili zilizosalia zitakazopigwa kati ya Juni 18 na 22.

Kagera iliyoshuka daraja ikishika nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu kwa sasa itakuwa wageni wa Namungo Juni 18 na Kaseja ameona hakuna sababu ya kwenda kukutana kambini mjini Bukoba na badala yake watajiandaa wakiwa Dar kwani watamalizia mechi na Simba Juni 22.

Kaseja alisema ameamua kuwaita wachezaji hao wakutane Dar keshokutwa Jumanne ili kuajindaa na mechi hiyo na Namungo kisha kumalizana na Simba kwenye Uwanja wa KMC  kufunga msimu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kaseja alisema wana dakika 180 ngumu ugenini, hivyo kutokana na hilo wameamua kuitana kambini Dar es Salaam ili kupunguza uchovu wa kuanzia safari kutokea Kagera kuifuata Namungo watakayokutana nayo Ruangwa mkoani Lindi.

“Ni kweli tuna hali mbaya kwa vile tumeshashuka daraja, lakini hilo halituondoi kwenye mstari kwa kuanza mazoezi haraka ili kujiweka tayari na mechi mbili zilizobaki malengo ni kuhakikisha tunafanya vizuri kwa kukusanya pointi zote sita,” alisema Kaseja na kuongeza:

“Jumanne tutakutana tayari kwa maandalizi tunaamini tutakuwa bora na kazi niliyonayo ni kuwajenga wachezaji wangu waweze kuipambania timu licha ya kuwa kwenye nafasi ambayo hairidhishi lakini heshima ya Kagera Sugar bado inathamani katika jezi zao.”

Kaseja alisema hawajiandai kwa ajili ya kukamilisha ratiba bali kwa lengo la kupambania timu hiyo ili isiwe daraja la timu nyingine kukusanya pointi kupitia timu hiyo iliyoiaga Ligi Kuu baada ya kuicheza kwa miaka 21 tangu ilipopanda mwaka 2004.