Simba yaichapa African Lyon

Mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) uliozikutanisha timu za African Lyon na Simba umemalizika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kwa Simba kuibuka na ushindiwa bao 3-0.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa Simba kwenda mapumziko wakiongoza kwa bao 2-0 zote

zikifungwa na Ibrahim Ajibu dakika ya 10 na 44.

Kipindi cha pili kimerejea kwa timu zote kucheza kwa utulivu na dakika zilivyozidi kwwnda Simba waliimarika zaidi kuliko Lyon na kurejea kwenye kutawala mpira kwa pasi fupi fupi.

Dakika ya 54 timu zote mbili zilifanya mabadiliko Simba wa kimtoa  HassanDilunga  na kuingia Miraji Athuman huku Lyon akiingia  Mwarami Abdallah kuchukua nafasi ya Geofrey Mwashuiya.

Kazi nzuri aliyofanya Miraji Athuman kwa kuwapiga chenga mabeki wa Lyon na kutoa pasi penyezo kwa Perfect Chikwende aliyefunga iliwapatia Simba bao la tatu 63.

Mabadiliko mengine yalifanyika dakika ya 70 kwa Simba kumtoa Rally Bwalya na kuingia Said Ndemla huku Lyon akitoka Rehani Kibingu na nafasi yake kuchukuliwa na Moris Kaniki.

Dakika ya 81 Simba walifanya mabadiliko mengine kwa kumtoa Meddie Kagere na nafasi yake kuchukuliwa na John Bocco.

Kassim Yusuph wa Lyon aliingia dakika ya 90 kuchukua nafasi ya Sadi Mtikila lakini hajaonesha madhara yeyote kwa Simba.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, African Lyon 0-3 Simba.

Matokeo haya yanawafanya Lyon kuaga mashindano hayo huku Simba wakisonga mbele katika hatua inayofuata.