Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yafika uwanjani, yatumia mlango usio rasmi

ZNZ Pict

Muktasari:

  • Katika hali ya kushangaza, kikosi hicho kimetumia mlango usio rasmi kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kikitumia mlango wa VIP ambapo ni kinyume na utaratibu.

Kikosi cha Simba kimewasili Uwanja wa New Amaan Complex saa 12:37 jioni tayari kwa mchezo wa Dabi ya Kariakoo utakaopigwa kuanzia saa 2:15 Usiku.

Katika hali ya kushangaza, kikosi hicho kimetumia mlango usio rasmi kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kikitumia mlango wa VIP ambapo ni kinyume na utaratibu.

Bodi ya Ligi wakati inafanya maandalizi ya mchezo huo, iliandaa maeneo maalumu ya wachezaji hao kuingia kwa timu zote mbili, Simba na Yanga kwa kuweka mabango ya wadhamini.

Yanga ilitumia mlango rasmi tofauti na Simba kama walivyoelekezwa.

Kutumia mlango usio rasmi ni kuvuna kanuni ya 17:21 ya Ligi Kuu Bara inayohusu Taratibu za Mchezo, adhabu yake ni faini ya Sh1 milioni.