Simba ya Mgunda balaa, kutesti mitambo Zenji

Summary

  • KLABU ya Simba leo imeenda visiwani Zanzibar kwaajili ya kambi maalumu ya siku tano na ikiwa huko itatesti kikosi chake kwa kucheza mechi mbili za kirafiki.

KLABU ya Simba leo imeenda visiwani Zanzibar kwaajili ya kambi maalumu ya siku tano na ikiwa huko itatesti kikosi chake kwa kucheza mechi mbili za kirafiki.

Mchezo wa kwanza itacheza Septemba 25, 2022 dhidi ya Malindi inayoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar mechi itakayopigwa katika uwanja wa Amaan kuanzia saa 2:15 usiku.

Mechi ya pili itakuwa dhidi ya Kipanga iliyofuzu kucheza hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiungana na Azam FC kutoka bara ambayo yenyewe imeanzia hatua ya kwanza.

Mechi dhidi ya Kipanga itapigwa Septemba, 28,2022 saa 2:15 usiku kwenye uwanja ule ule wa Amaan na baada ya hapo Simba itarejea Dar es Salaam kwa maandalizi ya muendelezo wa mechi za ligi na zile za CAF itakapoanza ugenini dhidi ya Primiero de Agosto ya Angola.

Baada ya kurejea Dar es Salaam itaendela kujifua kabla ya Oktoba 2, 2022 kujitupa uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza mechi ya ligi duru ya tano dhidi ya Dodoma Jiji kisha itasafiri kwenda Angola ambako mechi itapigwa  Oktoba 9, 2022.