Simba wakomaa na matuta hadi kieleweke
MATOKEO ya sare kwenye mechi mbili mfululizo zilizopita za dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga katika Ligi Kuu Bara msimu huu, zimewafanya Wekundu wa Msimbazi kujiandaa kukabili hatua ya kupigiana matuta kama mechi ya leo pia itamalizika kwa sare.
Kikosi cha kocha Pablo Franco kitawavaa mahasimu wao wa jadi Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) ambayo dakika 90 zikimalizika kwa sare, hazitaongezwa 30, bali moja kwa moja itaamuliwa kwa kupigiana penalti.
Kwa kutambua kuwa lolote linaweza kutokea, Simba imefanya mazoezi muhimu ya kupiga penalti na mambo yalikuwa ni moto.
Kila mchezaji alipiga penalti na yule aliyeonekana kukosa basi alirudia.
Ni Kibu Denis pekee ndiye aliyeonekana kukosea kila anaporudia hivyo alilazimika kurudia kupiga hadi alipopata.
Mshindi wa mchezo wa leo atacheza dhidi ya mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Coastal Union na Azam FC, ambazo zitakutana kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jij