Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba: Tunatibua kundi, ushindi ni Sh800 milioni

HESABU ya Simba ni moja tu leo, kuibuka na ushindi ugenini dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast na kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kujihakikisha mamilioni kutoka Caf na si vinginevyo.

Matokeo hayo yataifanya Simba ifikishe pointi 10 zitakazoivusha hadi robo fainali na kuandika rekodi ya kuwa ya kwanza kutoka Tanzania kutinga hatua hiyo tangu michuano hiyo ilivyobadilishwa 2004.

Mbali na kuweka rekodi, lakini itajihakikisha kuvuna zaidi ya Sh800 milioni zinazotolewa kwa timu inayotinga hatua hiyo.

Ushindi katika mechi hiyo itakayopigwa mjini Cotonou, Benin kuanzia saa 1:00 utaifanya Simba iwe na uhakika kuwa moja ya timu mbili za Kundi D kufuzu hatua inayofuata kwani Asec haitamaliza ikiwa na idadi hiyo. Sio Asec tu, bali hata US Gendarmerie ya Niger au RS Berkane ya Morocco zinazoumana leo hazitaifikia.

Simba inafahamu sio mechi rahisi na italazimika kupambana kupata ushindi kutokana na kiwango bora cha Asec katika mechi za hivi karibuni, lakini pia ubabe ikiwa nyumbani.

Katika mechi 10 za mwisho za kimataifa ilizocheza nyumbani Asec, imeshinda tisa na kutoka sare moja tu, ikifunga mabao 16 na kufungwa matatu.

Kudhihirisha benchi la ufundi la Simba linafahamu vyema ubora na ugumu wa Asec kufungika ikicheza nyumbani, kocha Pablo Franco amekiri wanatakiwa kucheza kwa tahadhali na nidhamu muda wote wa mchezo.

“Tutacheza kwa nidhamu kubwa hapo, kwani michezo miwili waliyocheza wametumia vizuri uwanja huo na kushinda,” alisema Pablo.

Kwa sasa Simba imeonekana kufanya vyema ugenini katika mechi za kimataifa tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma, huku nyota wake Pape Ousmane Sakho, Bernard Morrison, Meddie Kagere, Rally Bwalya na Peter Banda wakiwa gumzo, na Pablo akiwapa kazi maalumu ya kuizima tena Asec.

Kumbukumbu zinaonyesha katika mechi 10 zilizopita za CAF ambazo Simba imecheza ugenini, imeshinda tatu, sare tatu na kupoteza nne, ikifunga mabao matano na kuruhusu tisa.

Katika mechi ya leo, Simba inapaswa kuwa mastaa wawili wa Asec, Stephane Ki na Karim Konate ambao kwa pamoja wameifungia mabao matano kati ya sita iliyofunga. Ki ndiye aliifungia Asec bao pekee katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo jijini Dar es Salaam ambao Simba ilishinda mabao 3-1.

Kati ya mabao matano iliyopachika Simba, mawili imepata kipindi cha kwanza na matatu cha pili - wenyeji wao Asec wameonekana kuwa tishio zaidi kipindi cha pili, kwani kati ya mabao sita, manne wamepachika kipindi cha pili na mawili cha kwanza.

Kocha Pablo alisema kuwa wanaingia katika mchezo huo wakiwa na faili lililojitosheleza la taarifa za wapinzani wao kimbinu.

Kikosi kinachoweza kuanza ni Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein, Joash Onyango, Henock Inonga, Jonas Mkude, Peter Banda, Rally Bwalya, Meddie Kagere, Bernard Morrison na Ousmane Sakho.