Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, TFF ngoma nzito ishu ya GSM

Mangungu: Simba hatufanyi mipango nje ya Uwanja

KLABU ya Simba imeendelea kushikilia msimamo wake wa kutotumia nembo ya mdhamini mweza wa Ligi Kuu Bara kampuni ya GSM Tanzania Limited.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi (TPLB) imeeleza kuwa ilikutana na wenyeviti wa klabu mbalimbali kuhusu kujadili masuala ya udhamini wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22.

Katika kikao hicho kilichofanyika Desemba 17, viongozi hao wa vilabu walipata nafasi ya kushauriana na kukubaliana na Bodi ya Ligi kuhusu namna bora zaidi ya kutekeleza masharti ya mikataba ya udhamini kwa lengo la kuhakikisha wadhamini waliopo wanaridhishwa na utekelezaji lakini pia kuvutia wadhamini wapya.

Aidha taarifa iliongeza kuwa suala la kampuni ya GSM Tanzania ambao ni mdhamini mweza wa Ligi Kuu Bara Klabu 15, kati ya 16 zinazoshiriki Ligi hiyo zimetoka na azimio la kuendelea kutekeleza matakwa ya mkataba huo ikiwemo kuweka nembo ya GSM kwenye bega la kushoto la jezi zinazotumika kwa michezo ya ligi hiyo.

Klabu hizo 15 ni Geita Gold, Mtibwa Sugar, Mbeya Kwanza, Tanzania Prisons, Biashara United, Ruvu Shooting, KMC FC, Kagera Sugar, Namungo FC, Azam FC, Coastal Union, Dodoma Jiji, Polisi Tanzania, Mbeya City na Young African ambazo zimeridhika na utaratibu uliotumika katika kuingia mikataba yote ya udhamini msimu huu huku wakiziomba Bodi ya Ligi na TFF kuendelea na juhudi za kutafuta wadhamini zaidi.

Akizungumzia kutokuwemo kwenye timu zilizozibitisha kuvaa nembo hiyo Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu alisema kuwa walishatuma barua yao kwenda Bodi ya Ligi ya kutokubaliana na mkataba huo hivyo msimamo wao utaendelea kuwa pale pale.

"Kwa kauli moja kama viongozi tulishaamua kusimamia msimamo wetu kama klabu na hatuwezi kugeuza maamuzi, waliodhibitisha ni wao na sisi tutabaki na matakwa yetu," alisema Mangungu ambaye hakutaka kuweka wazi walichokiandika kwenye barua hiyo.

Wakati Simba wakishikilia msimamo huo Bodi ya Ligi imezishukuru Klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Bara msimu huu kwa ushirikiano wao katika kujadili changamoto na kutafuta majibu kwa pamoja huku ikizitaka kuendelea kutekeleza kikamilifu matakwa ya mikataba yote ya udhamini kwani jambo hili huvutia pia wadhamini wapya.

Katika hatua nyingine uongozi wa Benki ya NBC na mwakilishi wa kampuni ya kutengeneza mabasi ya Yutong, wamezungumza na mweyeviti hao wa klabu kuhusu utaratibu wa kukopeshwa mabasi ya kisasa kwa ajili ya safari za timu zao.

Klabu ambazo ziko tayari kukopa mabasi hayo zimetakiwa kutuma barua kwa Bodi ya Ligi ili mchakato huo ufanyike kupitia makubaliano kati ya Benki ya NBC na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).