Simba Queens bingwa tena

Sunday May 16 2021
bingwa pic
By Mustafa Mtupa

BADO wao. Ndio unaweza kuanza kuhesabu wakati Simba jike inajikamatia swala wake kule Dodoma aliyemsumbua kwa zaidi ya dakika 90.
Timu ya Wanawake ya Simba Queens jana ilinyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya kuibamiza Baobao Queens bao moja kwa sifuri lililofungwa na mshambuliaji wao Asha Djafari dakika za nyongeza.
Simba Queens ilihitaji matokeo ya kushinda tu, ili kuchukua ubingwa huo kutoka na tofauti ya alama iliyokuwepo kati yao na mpinzani wao Yanga Princess.
Kabla ya mchezo huo Simba ilikuwa inaongoza ligi kwa alama 51 baada ya kucheza mechi 19, wakati Yanga ilikuwa na alama 50 baada ya kucheza mechi 19 pia.
Jana zote zilikuwa dimbani Yanga ilijipinda dhidi ya Alliance Girls kwenye uwanja wa Karume, Ilala, Jijini Dar es salaam na Simba ilikuwa huko Dodoma dhidi ya Baobab na Yanga ikashinda mabao 6-0, lakini haikusaidia kwani imezidiwa na Simba alama moja ambayo ndio imeamua bingwa.
Huu unakuwa  ni msimu wa pili mfululizo kwa Simba kutwaa ubingwa  baada ya kufanya hivyo msimu uliopita pale kwenye dimba la Uhuru, Jijini Dar.

Advertisement