Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba ni wao tu kwa Mkongo

SIMBA Pict

MABOSI wa Simba sasa imebaki wao tu kuweza kumaliza kazi kwa kwenda ‘kuvunja’ benki ili kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji Mkongomani, Agee Basiala kutoka AS Union Maniema baada ya klabu hiyo ya DR Congo kuweka hadharani dau la kumuuza nyota huyo aliyewahi kutakiwa pia na Yanga.

Basiala anawindwa na Simba akitajwa kama mbadala sahihi iwapo Jean Charles Ahoua atasepa zake Afrika Kusini anakowindwa na Kaizer Chiefs inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi, baada ya kuonekana dili la kumnasa Feisal Salum ‘Fei Toto’ kuwa gumu.

Taarifa za ndani zililiambia Mwanaspoti mabosi wa Maniema wamekuwa wakizungumza na wenzao wa Msimbazi na tayari wamewekewa mezani dau la kuweza kumbeba na kilichobaki ni Simba kuamua moja kuingiza mkono mfukoni na kuwalipa ili waendelee na yao.

“Simba imepewa rasmi dau la kumpata kiungo huyo, huku ikitakiwa kumnunua kwa Dola 150, 000 (zaidi ya Sh390 milioni),” kilisema chanzo hicho makini na kuongeza;

“Kama itamuuza Ahoua kwenda Kaizer huenda ikapata pesa za kumnunua kiungo huyo ambaye atasimama kama mbadala kwa msimu ujao.”

Mwanaspoti lilizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa AS Maniema, Guy Kapya Kilongozi alisema, ni kweli Simba imewatafuta na tayari wameshawapa dau.

“Yuko bosi wa Simba ametutafuta anamtaka Agee (Basiala), tumewapa majibu yetu ya pesa ambazo wanatakiwa kutupa ili wamnunue na tufanye biashara. Wote mnajua Agee ni kiungo bora sana na sasa amekomaa kucheza kokote, hapa Maniema bado ni mtoto wa nyumbani tunamhitaji, lakini kama kuna ofa nzuri tutaisikiliza,” alisema Kilongozi na kuongeza;

“Tumeuza wachezaji wengi kwenda Tanzania, unamwona Maxi Nzengeli, ametoka hapa na wengine wengi, tumewaambia tunayotaka walikubali watakuja tutafanya biashara.

Hapo awali kupitia Mwanaspoti iliandika, kiungo huyo aliwahi kutakiwa na Yanga kabla ya Simba kutua kwa ajili ya msimu ujao.


KUHUSU AHOUA

Hivi karibuni Nabi alipokuwa nchini kwa mambo yake binafsi alishuhudia mchezo wa Simba dhidi ya Singida Black Stars uliopigwa pale KMC Complex, Wekundu hao wakishinda kwa bao 1-0, likifungwa na straika Mganda, Steve Mukwala.

Baada ya mchezo huo alivutiwa na kiungo Jean Ahoua kisha akatia neno kidogo mbele ya Mwanaspoti, kumbe hakuishia hapo tu, bali alimpa kazi maalum skauti mkuu wa Kaizer, Thembela Tera Maliwa, aliyemfuatilia zaidi katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) iliyopasuka 3-1 mbele ya Singida BS.


REKODI ZA BASIALA

Basiala ana uwezo wa kucheza kama winga na kiungo mshambuliaji, anasifika kwa kutoa pasi za mwisho na kuchezesha timu,lakini pia anatupia sana mipira ya adhabu kama Stephane Aziz KI aliyekuwa Yanga kabla ya hivi karibuni kuuzwa Wydad Casablanca ya Morocco.

Viungo na mawinga wanaocheza katika nafasi hiyo ni Mzamiru Yassin, Awesu Awesu, Joshua Mutale, Ladack Chasambi, Augustine Okejepha na Charles Ahoua.