Simba ni dhahama

Muktasari:

Mchezo wa kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Kaizer Chiefs umemalizika usiku huu Mei 15, 2021 kwa Simba kupoteza kwa mabao 4-0.

Mchezo wa kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Kaizer Chiefs umemalizika usiku huu Mei 15, 2021 kwa Simba kupoteza kwa mabao 4-0.

Matokeo hayo yanawaweka Wanamsimbazi pabaya katika ndoto za kukata tiketi ya hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Katika mchezo wa leo uliopigwa kwenye Uwanja wa FNB Afrika Kusini, Simba walizidia na kukubali kuruhusu mabao 4-0.

Ilichukua dakika 6 tu kwa wenyeji Kaizer Chiefs kuzifumania nyavu za Msimbazi kupitia kichwa cha Eric Mathoho huku Samir Nurkovic akitupia bao la pili dakika ya 34 kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Hadi timu zote zinakwenda mapumziko wenyeji Kaizer walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kuchangamka na kutawala mchezo lakini ilichukua dakika 12 tu baada ya kipindi cha pili kuanza, Kaizer kuandika bao la pili kupitia kwa Nurkovic ambaye bao hilo lilikuwa la tatu kwa klabu yake katyika mchezo huo.

Leonardo Castro alizidisha machungu kwa Wanamsimbazi kwa kuhitimisha bao la 4 katika mchezo huo bao ambalo alilifunga dakika ya 63 ya mchezo.

Matokeo hayo yameiweka njiapanda Simba katika mbio za kukata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali ambayo itatakiwa kushinda mabao 5-0 kwenye mchezo wa marudiano.

Mchezo wa marudiano utapigwa Jumamosi Mei 22, 2021 katika dimba la Mkapa jijini Dar es salaam.