Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba mguu pande, Okra

Simba mguu pande, Okra

MCHANA wa juzi Simba ilimtambulisha kiungo mshambuliaji, Mghana Augustine Okrah kama vile ambavyo Mwanaspoti lilikuwa la kwanza kukueleza kila kitu, huku mastaa wake wengine wakikaa mguu sawa kwa ajili ya kuanza kambi ya maandalizi ya msimu mpya.

Okrah aliyesaini mkataba wa miaka miwili akitokea Benchem United ya Ghana, lakini mastaa wote wa Simba waliopo nchini mchana wa juzi walifanya vipimo vya afya hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuanza maandalizi ya msimu mpya.

Zoezi hilo la kufanya vipimo vya moyo, damu, presha, uzito na vingine vingi vilifanyika ili Daktari wa timu hiyo, Edward Kagabo.

Miongoni mwa wachezaji waliokamilisha zoezi hilo la vipimo wapo majembe mapya, Okrah, Victor Akpan, Nassoro Kapama, Habibu Kyombo pamoja na Jonas Mkude, Aishi Manula, Shomary Kapombe na wengine. Wapo pia nahodha, John Bocco, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ aliyekuwa anakula bata Dubai na familia yake, Kennedy Juma na Clatous Chama.

Saa 3:00 asubuhi ya jana Alhamisi kocha wa Simba, Zoran Maki alitoa maelekezo wachezaji wote waliopo nchini awakute kambini bila kuchelewa hata sekunde ili kunywa chai ya pamoja kabla ya kuanza zoezi la utambulisho na vikao vya utaratibu wake wa kazi.

Baada ya chai, Zoran akiwa na baadhi ya viongozi wa timu atatambulishwa mbele ya wachezaji wote kila mmoja kumfahamu huku akipata nafasi ya kuongea nao. Kila mchezaji atapewa nafasi ya kujitambulisha majina yake mawili kama alikuwemo msimu uliopita atafanya hivyo na hata wale wapya nao wataeleza.

Zoezi la utambulisho baada ya kukamilika kuna vikao vitafanyika ikiwemo kuelezwa umuhimu wa kambi Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao kila mchezaji namna gani anatakiwa kujituma kwa ajili ya msimu ujao.

Baada ya hapo wachezaji, benchi la ufundi pamoja na viongozi walikula chakula cha mchana kisha kuanza safari ya kuelekea Uwanja wa ndege kwa ajili ya kuanza safari Misri.

Alipoulizwa kocha, Maki alisema wachezaji wanakwenda kufanya maandalizi ya kutosha ili kuhakikisha wanarejea nchini wote wakiwa katika utimamu mzuri wa mwili na kushindana katika michezo ya ushindani.

“Tunakwenda kuandaa timu kuhakikisha tunarudi katika michezo ya mashindano tukiwa katika kiwango bora ili msimu ujao kufanya vizuri kwenye mashindano yote kama malengo yetu yalivyo,” alisema Maki ambaye lengo lake kubwa ni kuifikisha Simba nusufainali ya Afrika kama alivyofanya na Wyadad Casablanca ya Morocco.