Simba: Manula yupo fiti kucheza

Klabu ya Simba imesema golikipa Aishi Manula amepona jeraha lake baada ya kufanyiwa upasuaji wa nyama za paja na sasa yupo fiti kucheza.
Manula aliumia katika mechi ya robo fainali ASFC dhidi ya Ihefu na amekaa nje ya uwanja kwa takribani miezi minne na tayari amefanya mazoezi na wenzake.
"Kwa sasa Manula yupo fiti kuanza kushuka dimbani kutegemea na uhitaji wa benchi la ufundi ingawa anatakiwa kuendana na kasi ya mazoezi na wenzake," imeeleza taarifa ya Simba
Simba itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu kwa Tanzania Prisons kwenye mechi ya Ligi Kuu Alhamisi Oktoba 5.