Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba Day rasmi Agosti 28, waweka kambi ya kishua

SIMBA wametangulia kwenye kambi ya kishua. Waliondoka Jijini Dar es Salaam jana mchana kuelekea kambini nchini Morocco huku Yanga ikipanga kufanya hivyo Jumatatu asubuhi.

Mwanaspoti limebaini kwamba timu hizo mbili zinakwenda kwenye miji ambayo ipo katika tano bora za ufahari na utajiri nchini humo, jambo ambalo limefanya timu kadhaa za Afrika kuzidi kuwahofia.

Awali Simba ilikuwa iweke kambi kwenye Jiji la Alexandria, Misri lakini wakaamua kuhamisha baada ya kubaini kulikuwa na changamoto ambazo zingeweza kuwakwamisha .

Uchunguzi uliofanywa na Mwanaspoti nchini humo umebaini kwamba Simba inatua kwenye mjini wa Rabat huku Yanga ikielekea Casablanca. Miji hiyo yenye miundombinu ya kisasa ya michezo iko umbali wa saa moja kwa usafiri wa barabara na treni.

Mmoja wa viongozi wa Yanga, Haji Mfikirwa aliithibitishia Mwanaspoti jana kwamba wanakwenda kambini Jumatatu licha ya kwamba hakutaja eneo wala hoteli.

Kwa mujibu wa takwimu za kitalii nchini humo, Marrakech ni mji wa kwanza kwa ufahari na gharama, Tangier wa pili, Casablanca wa tatu, Rabat ya nne na Agadir ukiwa wa tano.

Tathmini inaonyesha licha ya kwamba hoteli nyingi zimeruhusiwa kuchukua asilimia 70 tu ya uwezo wake kutokana na corona, lakini bado maisha ni ghali kwenye hoteli na miji hiyo na kumudu kusafirisha na kuweka kambini kundi la watu ni mamilioni ya shilingi.

Lakini tathmini ya watembezi inaonyesha kwamba hakuna tofauti kubwa kati ya Casablanca na Rabat zinakoenda kupiga matizi ya wiki mbili timu hizo nguli.

Simba na Yanga zinajiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika inayoanza Septemba 11 ambayo itakuwa ni kabla ya Ligi Kuu Bara kuanza.

Habari zinasema kwenye miji hiyo hakuruhusiwi mikusanyiko ya zaidi ya watu 25 kutokana na corona lakini wale waliochanjwa wamepewa upendeleo maalum wa kuongezewa masaa ya kusafiri.

Simba watakaporudi watafanya Simba Day ambayo hutumika kutambulisha wachezaji wao wapya na shughuli mbalimbali za timu.