Show Show! Dakika 90 Yanga vs Simba
Hawatuwezi ndivyo mashabiki wa Simba walivyojipanga wakiimba baada ya beki Joash Onyango kusawazisha bao dakika ya 86 na kuleta shangwe kwa mashabiki hao ambao walikuwa wamepoa muda mwingi wa mchezo.
Bao hilo lilikuwa la kusawazisha baada ya Michael Sarpong kuitanguliza Yanga kwa bao la penalti dakika ya 31.
Yanga ilionyesha soka safi katika mchezo huo muda mwingi wa mchezo jambo lililosabbisha mashabiki wa Simba kuwa wanyonge.
Kitendo cha kocha wa Yanga Cedrick Kaze kumtoa Surpong dakika 60 na kumuingiza Yacouba Sogne, kiliwapunguzia kazi mabeki wa Simba, Pascal Wawa na Joash Onyango na kuanza kupanda mbele kutafuta bao la kusawazisha kwa timu yao.
Sarpong aliwapa wakati mgumu mabeki hao kwani alikuwa hodari katika kuficha mpira mguu huku akiwa na kasi.
Yanga ilionyesha soka safi zaidi ya Simba hasa kipindi cha kwanza hivyo kuonekana kama ilipania kuwathibitishia Wekundu wa Msimbazi kuwa wamefanya usajili wa maana msimu huu licha ya mwanzo kuwabeza.
Licha ya Yanga kusifika kwa kucheza pasi ndefu wanapokwenda kushambulia lakini ilionekana kucheza pasi fupi na za maelewano na kuamsha shangwe kwa mashabiki wao waliofika kwa wingi uwanjani.
Safu ya kiungo ya Yanga ilionekana kucheza vizuri ikiwa chini ya Mukoko Tonombe na Feisal Salum ambao waliwapoteza kabisa viungo wa Simba Rally Bwalya, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na Clatous Chama.
Viungo wa Simba licha ya kuwa ni wazuri kwa kucheza mpira lakini walikosa ubunifu wa kupeleka mashabulizi kwa mshambuliaji wao John Bocco ambaye kuna wakati alikuwa akirudi nyuma kutafuta mpira.
Pia kasi ya Tuisila Kisinda aliyecheza kama winga wa kulia ilimpa wakati mgumu beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye alitumia nguvu kubwa kumdhibiti.
Tuisila ila ni mchezaji mwenye kasi ambaye kila alipopata mpira alikuwa akitoka spidi kupeleka mashambulizi langoni kwa Simba hadi kusababisha penalti iliyozaa bao kwa timu yake baada ya kukwatuliwa na beki Joash Onyango ndani ya eneo la hatari.
Mchezo ulivyokuwa
Yanga ilianza mchezo kwa kasi ikionyesha kuwa imepania kushindanmchezo huo na dakika ya 3 tu walifika golini kwa Sikba na shuti la Michael Sarpong likaokolewa na mabeki wa Simba
Dakika ya tisa Yanga ilipata kona iliyopigwa na Farid Mussa lakini kipa Aishi Manula aliokoa na kuwa kona nyingine tasa
Simba iliamka na kufanya shambulizi zuri golini kwa Yanga na kupata faulo nje kidogo ya 18 baada ya beki Lamine Moro kumkwatua Shomari Kapombe na faulo hiyo kupigwa na Larry Bwalya na kuokoleaa na mabeki wa Yanga mabao walianzisha shambulizi la kustkukiza kuelekea golini kwa Simba hata hivyo Jonas Mkude akaokoa.
Dakika ya 13 Sikba ilipata kona iliyopigwa na Mohammed Hussein Tshabalala ambayo iliokolewa na Moro.
Yanga iliendelea kucheza vizuri na dakika ya 13 wachezaji wa timu hiyo waligongeana vizuri pasi mpira kumkuta Tuisila ambaye alishindwa kufunga akibaki yeye na kipa Aishi Manula ambaye aliokoa kwa miguu kisha kuudaka mpira huo
Dakika ya 18 Simba ilipata faulo iliyopigwa na Pascal Wawa ambaye alipaisha kabla ya Yanga nao kupata faulo nje kidogo ya 18 dakika moja baadae iliyopigwa Farid Mussa na mabeki wa Simba kuokoa.
Pia Simba ilipata faulo nyingine nje ya 18 dakika ya 23 na 26 lakini wachezaji wake Larry Bwalya na Clatous Chama walishindwa kufunga.
Kipindi cha pili Simba ili fanya mabadiliko kwa kumtoa Larry Bwalya na Mzamiru Yassin na kuwaingiza Hassan Dilunga na Ibrahim Ajib wakati Yanga ilimtoa Michael Sarpong na Farid Mussa na kuwaingiza Yacouba Sogne na Zawadi Mauya.
Mabadiliko hayo ya Lionel ana kumbe a zaidi Simba kwani dakika za mwisho. Ili changa ka na kupata bao la kusawazisha.
Sven amsababishia kadi Manula
Kadi ya njano aliyopewa kipa wa Simba, Aishi Manula dakika ya 30 ni kama ilisababishwa na kocha wake Sven Vandenbroeck.
Baada ya Yanga kupata penalti kabla hawajapiga penalti hiyo Manula alitoka golini na kwenda karibu na benchi la Simba kisha kuongea na kocha wake.
Wakati wakiendelea kuongea beki wa Yanga Lamine Moro alionekana kuwafuata akisikiliza mazungumzo yao na ndio Sven alipomvuta Manula na kumtoa nje kabisa ya mstari wa uwanja.
Wakati akirudi golini ili kujiandaa kupigiwa penalti hiyo mwamuzi Abdallah Mwinyimkuu wa Iringa alimzawadia kadi ya njano kwa kosa la kutoka nje ya uwanja bila ruhusa.