Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shabiki wa Madrid, Yanga asomba mamilioni

SHABIKI wa Real Madrid, Yanga Jacob Mkungilwa kutoka mkoani Njombe ameibuka kidedea baada ya kujishindia Sh112 milioni kupitia ubashiri wa kampuni Premier bet Navigator.

Mkungilwa ameshinda fedha hizo kupitia ubashiri wa michezo ya soka iki ni ushindi wake mkubwa tangu aanze kucheza michezi hiyo ambapo sasa anataka kujiendeleza zaidi.

Mkungilwa ambaye anafanya biashara ya kulangua mahindi makavu alisema fedha hizo sasa zitakwenda kuinua maisha yake kwa kuanzia bishara zingine zitakazokwenda kujipatia kipato zaidi

"Mara ya kwanza nilipoona nimeshinda sikuamini, nilizima simu yangu na kuwasha tena bado nikaona ujumbe ni uleule kwamba nimeshinda hizo fedha, huu niu mtaji mwingine kwangu kwenda kujiimarisha kibiashara zaidi," amesema Mkungilwa

Naye Meneja biashara wa kampuni hiyo, Joy Chwaifaty alisema wito wao kwa mshindi huyo ni kwenda kutumia fedha hizo katika kujiinua kimaisha na sio kwewnda kutumia vibaya.

"Wako wengi wanashinda lakini tunachotaka ni kuona washindi kama hawa kina Jacob (Kungilwa) wanakwenda kujiinua kimaisha kama alikuwa anafanya biashara basi akainua biashara zake zaidi," amesema Chwaifty