Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shabiki aliyemlilia Ali Kiba azawadiwa Krismasi

Muktasari:

Msanii Ali Kiba ametoa ofa tya tiketi za bure kwa mwanamke aliyemlilia siku alivyokuwa akifanya show katika tamasha la Fiesta, lililofanyika viwanja vya Posta.

Dar es Salaam.Ikiwa zimepita siku mbili tangu dada anayejulikana kwa jina la Emiliana Mgema, kumlilia msanii Ali Kiba, akiwa anaimba katika tamasha la Fiesta, hatimaye msanii huyo amemuona na kutoa ofa kwake.
Katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagrama Ali Kiba alitangaza ofa hiyo huku akiwa ameweka video ya dada huyo akiwa anahojiwa huku analia na kueleza hisia zake jinsi anavyompenda msanii huyo.
Kiba aliandika ’ Asante sana dada anayemjua huyu dada amwambie nina tiketi yake ya bure na mofaya zake zakutosha tarehe 29 /12 Next Door Arena,”aliandika Kiba wakati anatangaza ofa hiyo kwa Emilina ambapo anatarajia kufanya shoo yake aliyoipa jina la ‘Funga mwaka na Ali Kiba’.
Mwananchi leo Desemba 25 ilimtafuta Emiliana ili kujua namna alivyopokea ofa hiyo ambaye amesema’Nimefurahisha sana japokuwa hata kama asingenipa ofa nilikuwa nimeshapanga kwenda.
Hata hivyo amesema kwa furaha aliyokuwa nayo baada ya Ali Kiba kumtambua na kumpa ofa hiyo, sasa badala ya kwenda usiku atafika saa nne asubuhi ili kuweza kuwahi nafasi ya mbele.
Katika hatua nyingine amewataka mashabiki waelewe kwamba anampenda Ali Kiba kwa kazi yake ya muziki na si vinginevyo kama wanavyofikiria na kauhidi kwamba siku ya onyesho lake kama atakwenda na mkewa pia atamwambia hilo ili asije akawa na wasiwasi naye.
Emy amesema ameanza kumpenda Ali Kiba tangu alipotoa kibao chake cha Macmuga ambapo kipindi hicho alikuwa akisoma darasa la saba katika shule ya Msingi Nata Mkoani Tabora, na kuanzia hapo amekuwa akimfuatilia hadi leo na hakuna ngoma yake hata moja aliyowahi kuiona mbaya.