Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti yakwama, Nigeria Safi

Muktasari:

  • Uganda ambao ndio Mabingwa wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, walianza mchezo huo kwa kasi ikiwabana Serengeti iliyomchezesha kipa Shaaban Hassan badala ya Mwinyi Yahya na kupata mabao yake kwenye kipindi hicho cha kwanza.


WAKATI safari ya Serengeti Boys kwenda Brazil ikipata vigingi baada ya jana Jumatano kupoteza tena mchezo wake wa Kundi A wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika U17 mbele ya Uganda, timu ya Nigeria imekuwa timu ya kwanza kufuzu nusu fainali ya michuano hiyo kwa kuichapa Angola bao 1-0.

Licha ya kucheza nusu fainali, Nigeria pia imekata tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia U17 kwa mara ya 12 baada ya kukusanya pointi sita katika mechi zake mbili, ikiwamo ile dhidi ya Serengeti walioinyoosha kwa mabao 5-4 katika mechi ya ufunguzi.

Nigeria ilikata tiketi hiyo katika mchezo wa kwanza uliopigwa jana mchana baada ya Olakunie Junuior kufunga bao pekee katika dakika ya 20, huku nyota wao, Samson Okikiola akiibuka nyota wa mchezo huo.

Angola ambao walianza michuano hiyo kwa kuichapa Uganda kwa bao 1-0, inaweza kujilaumu kwa kushindwa kuambulia hata sare kwani walitengeneza nafasi kadhaa lakini ilishindwa kuzitumia vyema.

Katika mchezo wa jioni, wenyeji Serengeti Boys ilishuka ikiwa imefanyiwa mabadiliko tofauti na kikosi kilicholala 5-4 mbele ya Nigeria, lakini bado haikuwasaidia vijana hao wa Taifa kuambulia angalau pointi katika kundi lake kwa kucharazwa mabao 3-0 na Uganda.

Uganda ambao ndio Mabingwa wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, walianza mchezo huo kwa kasi ikiwabana Serengeti iliyomchezesha kipa Shaaban Hassan badala ya Mwinyi Yahya na kupata mabao yake kwenye kipindi hicho cha kwanza.

Kocha Oscar Mirambo aliwaanzisha viungo Ladaki Chasambi na Edson Mshirakandi badala ya Mustafa Nankuku na Misungwi Chananja, lakini haikusaidia kuwazuia vijana wa Uganda waliomtumia winga wao Rogers Mugisha kutengeneza mashambulizi mengi.

Dakika 16 Uganda ilipata goli kupitia kwa Kawooya Andrew, huku dakika ya 28 Arafat Swakali aliiandikia bao la pili Uganda. Kipindi cha pili, Serengeti ilikuja kivingine na kuwabana Uganda, lakini haikusaidia kitu kwani dakika ya 76 jahazi liliendelea kuzama baada ya Najib Yiga kufunga bao la tatu kwa kichwa kutokana na mabeki wa Tanzania kujichanganya.