Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti yajifua kimbinu, Milambo afunguka kila kitu

Muktasari:

Baada ya zoezi hilo Milambo aliwapa wachezaji wake zoezi la kurusha mipira (Throw In) lakini aliwataka wasirushe mipira kwa nyuma badala yake warushe kwa kasi kuelekea kwa wapinzani wao na aliwataka washambuliaji wake Kelvin John na Maurice Abraham wasiwe na mambo mengi wanapokaribia golini.

BAADA ya kukamilisha zoezi la kushambulia kwa kasi, Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Milambo amehamia kwenye zoezi la kucheza mipira ya faulo.

Katika mazoezi yanayoendelea kwenye Uwanja wa JK Youthpark, Milambo aliwapa zoezi maalumu wachezaji wake kwa ajili ya kuwafanya wawe wpesi kupiga krosi lakini vilevile kwenye uokoaji.

Aliwataka wachezaji wake kupiga krosi ndefu na fupi kwa ufasaha na zoezi hilo lilipokuwa linakosewa walikuwa wanarudia mpaka wapatie.

Kwa upande wa mabeki waliokuwa wanacheza faulo hizo, walikuwa wanatakiwa kuokoa mashambulizi kwa uharaka ili adui asipate muda wa kucheza mpira langoni mwao.

Makipa nao walikuwa na kazi muhimu ambapo muda wote Manyika Peter alikuwa makini kuwaelekeza kucheza mipira ya krosi.

Baada ya zoezi hilo Milambo aliwapa wachezaji wake zoezi la kurusha mipira (Throw In) lakini aliwataka wasirushe mipira kwa nyuma badala yake warushe kwa kasi kuelekea kwa wapinzani wao na aliwataka washambuliaji wake Kelvin John na Maurice Abraham wasiwe na mambo mengi wanapokaribia golini.

Baada ya mazoezi hayo kumalizika Mwanaspoti lilizungumza na Milambo ambaye alisema amekuwa akifanya mazoezi hayo kuhakikisha kikosi kinakuwa bora kila eneo.

“Nataka kikosi changu kiwe bora kila eneo ambalo tunacheza, kuna makosa tuliyafanya Uturuki kwa hiyo nazidi kuyafanyia marekebisho, tunaendelea vizuri kila kitu kitakuwa sawa,” alisema.