Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti Boys yasaka Sh167Mil kwa Niger

Muktasari:

Mchezo huo dhidi ya Niger, umeshikilia hatma ya Serengeti Boys kuingia hatua ya nusu fainali kuhakikishia nafasi ya kushirki Kombe la Dunia litakalofanyika Oktoba huko India.

Dar es Salaam. Mbali ya kupata tiketi ya kushirki Kombe la Dunia kwa vijana wenye miaka 17, matokeo ya sare au ushindi kwa timu ya vijana ya Tanzania 'Serengeti Boys' dhidi ya Niger leo, timu hiyo itafanikiwa kupata zaidi ya Sh167 milioni iwapo itafuzu nusu fainali.

Mchezo huo dhidi ya Niger, umeshikilia hatma ya Serengeti Boys kuingia hatua ya nusu fainali kuhakikishia nafasi ya kushirki Kombe la Dunia litakalofanyika Oktoba huko India.

Kwa mujibu wa mgawanyo wa mapato kwa washindi wa mashindano mbalimbali yanayoandaliwa na shirikisho la soka Afrika (Caf), kila timu inayoingia hatua ya nusu fainali ya mashindano ya vijana wenye miaka 17, inatakiwa kupata kitita cha Dola 75,000 (zaidi ya Sh.167 milioni).

Ikitokea Serengeti Boys ikatwaa ubingwa wa mashindano hayo, itaondoka na kiasi cha Dola 150,000 ( Sh.335 milioni) wakati ikishika nafasi ya pili itavuna kiasi cha Dola 100000 (Sh. 223 milioni).  

Lakini hata ikitokea Serengeti Boys imeshindwa kufuzu hatua ya nusu fainali bado haitoondoka patupu bali itaondoka na kifuta jasho kulingana na nafasi itakayomalizia kwenye kundi lake.

Kama ikimaliza ikiwa kwenye nafasi ya tatu, itapatiwa kiasi cha Dola 60,000 (Sh.134 milioni) wakati kama itamaliza ikiwa ya mwisho kwenye kundi lake, itapata kiasi cha Dola 50,000 (Sh.112 milioni).

Kocha msaidizi wa Serengeti Boys, Oscar Milambo alisema kuwa kinachoangaliwa kwa sasa ni kufuzu kombe la dunia kama lengo kuu lililowekwa kabla hata ya mashindano hayo kuanza.

"Tunafahamu ugumu wa mechi ya mwisho dhidi ya Niger kwa sababu kila timu kwenye kundi letu ina nafasi ya kufuzu nusu fainali kutegemeana na matokeo ya mechi ya mwisho.

"Tulichopanga ni kuhakikisha tunaibuka na ushindi tu kwenye mchezo huo na sio vinginevyo kwa sababu ndio njia rahisi kwetu kutimiza lengo la kufuzu Kombe la Dunia," alisema Milambo.
xxxxxxxx
Mbao FC vs Yanga SC-CCM Kirumba, Mwanza
WAAMUZI
C. R: Ludovick Charles-Tabora
Line1-Makame Mdogo-Shinyanga
Line2-Vicent Mlabu-Morogoro
4th Official: Ferdinand Chacha-Mwanza
*****
KIKOSI CHA MBAO FC
Benedict Haule, David Mwasa, Asante Kwasi, Yussuf Ndikumana, Salmin Hozza, Jamal Mwembeleko, Ibrahim Njohole, Pius Buswita, George Sangija, Boniphace Maganga na Habib Haji
Akiba
Mussa Mohamed Musasa, Alex Ntiri, Steven Kigocha, Ndaki Robert, Dickson Ambundo, Vicent Philipo, Nelson Steven
Kocha Mkuu: Ettiene Ndayiragije
Kocha Msaidizi: Idd Slim
#####
KIKOSI CHA YANGA SC
Kipa Beno Kakolanya, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Vincent Bossou, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Justine Zulu, Obrey Chirwa, Haruna Niyonzima, na Geoffrey Mwashiuya
Akiba
Geogratius Munishi, Hassan Hamis, Pato Ngonyani, Deus Kaseke, Matheo Anthony, Emmanuel Martin
Kocha: George Lwandamina
Kocha msaidizi: Juma Mwambusi