Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti Boys hadi kieleweke

KOCHA Mkuu wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo amesema kikosi chake bado kina nafasi ya kutinga nusu fainali katika mashindano ya vijana chini ya miaka 17 ya AFCON yanayoendelea jijini Dar es Salaam lakini akaweka wazi suala la yeye kung’atuka ndani ya kikosi hicho.

Mirambo na kikosi chake wanahitaji miujiza sasa ili kusonga mbele baada ya kupoteza mechi mbili za kwanza za hatua ya makundi ya fainali hizo zinazofanyika nchini kwa mara ya kwanza.

“Matokeo tuliyopata awali ni yale tuliyokuwa na matarajio nayo. Tumeshindwa kutimiza ahadi. Si jambo zuri kwetu na inauma, lakini pamoja na hayo, si mwisho wa dunia, tunahitaji kila siku kujifunza kutokana na makosa ili kukaa kwenye mstari,” alisema Mirambo.

“Tunatakiwa kukaa sawa kwa kuangalia mechi yetu ijayo dhidi ya Angola inakuwaje. Hatuoni kama tumetoka kwa sababu tukishinda tutakuwa na pointi tatu, Nigeria wakiwafunga Uganda watakuwa na pointi tisa. Kutokana na hilo timu yetu, Angola na Uganda tutakuwa na pointi sawa tatu kila moja na kitakachofuata ni hesabu za mabao ya kufungwa na kufunga.”

Akizungumzia vijana wake, Mirambo amesema: “Upande wa watoto katika ufundi bado kuna kazi ya kufanya, hatupaswi kukata tamaa tumefanya lakini tunatakiwa kufanya zaidi na mwisho wa siku watu watambue kuwa tunawatengeneza wachezaji kwa ajili ya manufaa ya taifa, watuunge mkono.”

Akizungumzia nafasi yake ndani ya timu, Mirambo amesema: “Siko sawa kwa sababu unapofanya kazi unategemea matokeo mazuri. Jambo la kung’atuka au kutong’atuka si ishu kwangu au kuweka mezani na kujadili mbele ya watu. Kitu kinachofuata kwangu ni njia ya kutatua matatizo”

Alisema, hakujipa nafasi ya kufundisha Serengeti Boys na hata matokeo yaliyotokea hakuyapanga na hakuna aliyetaka, hivyo hawezi kufikiri jambo la kung’atuka katika kikosi hicho zaidi ya kujipanga kwa ajili ya mechi hiyo ijayo kwa sababu ndiyo itakayompa furaha watakaposhinda pamoja na Watanzania wote.

Tanzania inashika mkia katika Kundi A la michuano hiyo baada ya kulala 5-4 dhidi ya Nigeria na 3-0 dhidi ya Uganda.