Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti Boys bado nafasi ipo Afcon U17, msingi ni kupambana

Muktasari:

  • Wakati mwingine soka ndivyo lilivyo na hasa ikizingatiwa kuwa, Nigeria sio timu ya kubezwa kwani wana rekodi ya kushiriki fainali hizo mara nane, huku kwenye Kombe la Dunia U17 imeshiriki mara 11.

MICHUANO ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) U17 kwa mwaka 2019 imeanza kwa wenyeji Tanzania kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Nigeria.

Kipigo hicho kimewachanganya mashabiki wa soka ambao walikuwa na kiu ya kuona timu yao ya Serengeti Boys ikianza vizuri ili kujitengenezea mazingira ya kufuzu nusu fainali na kukata tiketi ya Fainali za Kombe kla Dunia U17 zza mwaka huu zitakazofanyika Brazili.

Wakati mwingine soka ndivyo lilivyo na hasa ikizingatiwa kuwa, Nigeria sio timu ya kubezwa kwani wana rekodi ya kushiriki fainali hizo mara nane, huku kwenye Kombe la Dunia U17 imeshiriki mara 11.

Nigeria U17 imetwa taji la Afcon mara mbili 2001 na 2007 wakati kwenye Kombe la Dunia imebeba mara tano 1985 ilipofanyika kwa mara ya kwanza, 1993, 2007, 2013 na 2015 kuonyesha Golden Eaglets sio timu nyepesi na hata matokeo ya 5-4 iliyopata Serengeti inastahili kupongezwa, japo imepoteza.

Lakini pia kipigo hicho hakipaswi kuwafanya vijana hao wa Serengeti na hata mashabiki wa soka nchini kukata tamaa. Tanzania bado ina nafasi ya kusahihisha makosa kwa mechi zao mbili zilizosalia katika Kundi A lenye Nigeria, Angola na Uganda.

Kesho Jumatano, Serengeti itavaana na Uganda katika mchezo wa pili, bahati mbaya zote zimetoka kupoteza mechi zao za awali, kwani Uganda walifumuliwa bao 1-0 na Angola hivyo kulifanya pambano hilo kuwa gumu kwa timu zote hususani wenyeji.

Kwa kuwa ni mechi hiyo na ile ya mwisho kundini dhidi ya Angola ndiyo zilizoshikilia hatma ya wenyeji kuvuka raundi ya inayofuata ya nusu fainali ambayo pia inatoa tiketi ya kucheza fainali za Brazili, ni wazi vijana wa Serengeti lazima wakaze mzuri. Kama alivyosema Kocha Mkuu wa timu hiyo, Oscar Mirambo kwamba ni lazima wapambane katika mechi hizo za mwisho kupata matokeo, ndivyo ambayo Serengeti wanapaswa kufanya. Hakuna njia nyingine ya kuwapa raha mashabiki ila kushinda dhidi ya Uganda na pia kwa Angola.

Alama tatu ni muhimu kwa mchezo wa kesho kwani ndio utaamua kama wenyeji tuendelee kuwepo kwenye michuano hii ama la, ndio maana tunawahimiza wachezaji kujitoa kama walivyojitoa dhidi ya Nigeria ili wapate matokeo. Kadhalika mashabiki wajitokeze kwa wingi na kuwapa sapoti vijana hao ili wapate matokeo na kuivusha Tanzania. Itakuwa aibu kama wenyeji watang’olewa mapema na kuwaacha wageni wapigane kuwania ubingwa.

Mwanaspoti kama wadau wakubwa wa michezo hususani soka, tunaamini Serengeti haitawaangusha mashabiki na mashabiki hawataiacha solemba Serengeti Boys katika mechi mbili muhimu zilizosalia.

Kama wenyeji tunapaswa kushikamana, kujitoa na kupambana kwa kila hali kuhakikisha tunapata matokeo yatakayoipa heshima nchi yetu, lakini pia kusaidia kulitangaza soka letu na kufungua milango ya soko la vijana wetu katika soka la kimataifa.

Bahati nzuri ni kwamba serikali juzi ilitangaza kuanzia jana Jumatatu, mechi zote za fainali hizo zitakuwa hazina viingilio ili kutoa nafasi kwa mashabiki kuhudhuria kwa wingi kwa nia ya kuunga mkono juhudi zilizochangia kuletwa kwa fainali hizo nchini kwa mara ya kwanza.

Hivyo basi wakati mashabiki wakifurahia kutotozwa viingilio, Serengeti nao wanapaswa kuongeza furaha kwa kupata matokeo mazuri kesho na mechi ya mwisho ya Angola ili Tanzania iandike rekodi ya kwanza ya kucheza nusu fainali ya michuano hiyo na kwenda Brazili katika fainali za Kombe la Dunia.

Kama mwaka juzi 2017 Serengeti ilishindwa kupenya Gabon kwenda katika fainali za Dunia nchini India tunadhani huu ni wakati wa Tanzania kuandika rekodi mpya kwao na soka la Afrika kwa kwenda Brazil na nafasi ipo kama tu vijana wataisimamisha Uganda na kisha Angola. Hizi ni mechi za kufa au kupona! Tunaamini, kama makocha wataenda kuufanyia kazi upungufu ulioonekana kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Nigeria hasa eneo la ulinzi na kipa, ni wazi Serengeti itaweza kufanya vema na kuwapa raha mashabiki na Watanzania kwa ujumla ambao kwa sasa wanachekelea timu yao ya taifa, Taifa Stars kufuzu Fainali za Afrika (Afcon) 2019 zitakazofanyika Misri.

Kila la heri Serengeti Boys, nafasi bado ipo na kipigo cha Nigeria kisiwakatishe tamaa kwani soka ni mchezo wa makosa na bahati, vijana wetu wajipange tu.