Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saido: Tulieni tupige kaziiiii!

Moto mpya Yanga ni noma

STAA mpya wa Yanga, Saido Ntibazonkiza amewaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba wala hawapaswi kupaniki na maneno ya mitandaoni kwani wao wachezaji wanajua nini cha kufanya.

Saido ambaye ni raia wa Burundi ni miongoni mwa wachezaji watatu waliosajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu Bara na Yanga. Wengine ni Mrundi mwenzie, Fiston Abdul Razak na mzawa, Dickson Job.

Straika huyo mzoefu na mechi kubwa amewasisitiza mashabiki wa Yanga kwamba mchezaji kutofunga siku moja isiwatishe bali waangalie ubora wake uwanjani na tachi zake zilivyo na macho na madhara makubwa.

“Watu wasivunjike moyo kwa matokeo ya mechi ya kirafiki, tutafanya vizuri kwenye mechi ijayo mbele yetu.Mashabiki wazidi kutusapoti sisi kila mechi kwetu itakuwa kama fainali,tutatumia akili na nguvu zetu zote kufikia kwenye malengo ambayo tunayahitaji,”alisema.

Kuhusu hali yake ya kiafya na kama atacheza mechi na Mbeya City alisema anaendelea vizuri na kadri siku zinavyoelekea atajua kama atacheza.

Ingawa Kocha wake, Cedrick Kaze alisema jana kwamba uwezekano wa kucheza Saido kwenye mechi ya wikiendi dhidi ya Mbeya ni hamsini kwa hamsini lakini kikosi chake kina wachezaji wengi wa kuamua matokeo.

Kuhusu ubora wa Fiston, Saido alisema kwamba mashabiki wawe watulivu na wasimhukumu kwa mechi moja tena ya kirafiki kwani inapofika katika mashindano huwa wanakuwa na mkakati tofauti kabisa.

Alisema kwamba itakuwa siyo sahihi kumpima Fiston kwa kutumia mechi ya kirafiki dhidi ya African Sports akawasisitiza mashabiki warudie kuangalia tachi zake uwanjani ndipo watakapoelewa ubora wake.

Kitendo cha Yanga kupoteza mechi ya kirafiki dhidi ya Sports kimeonekana kuwadhohofisha mashabiki wao kutokana na kejeli wanazozipata kutoka kwa wenzao wa Simba.

Awali Yanga ilikuwa haijapoteza mchezo wowote kwenye mashindano yote msimu huu, ingawa Kaze alikiri walipoteza kutokana na ugumu wa mazoezi ya wiki iliyopita ambayo yalikuwa lazima kujiweka sawa kwa mzunguko wa pili.