Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sadio Mane atoboa siri ya kuitosa Man U

LIVERPOOL, ENGLAND. Mshambuliaji Sadio Mane amesema kwamba kwa sasa angekuwa mchezaji wa Manchester United kama angeshawishika na maneno ya Louis van Gaal, lakini kwa wakati huo kitu ambacho alimjibu kocha huyo Mdachi kwamba "hawezi kwenda kujiunga na timu ya hovyohovyo."

Staa huyo wa Kisenegali, Mane alisema alifuatwa na kocha wa Man United kwa wakati huo, Van Gaal, kipindi hicho akiwa Southampton akimtaka aende akajiunge na wababe wa Old Trafford, lakini aliona haikuwa klabu sahihi kwake kwenda kuitumikia.

Mane kwa sasa anakipiga kwenye kikosi cha Liverpool na kwamba tayari msimu huu ameshatupia wavuni mabao matatu ikiwa ni jitihada zake za kuifanya timu yake kuchuana na Manchester City kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.

Mane alisema: "Sikuamini, kwa sababu kuna klabu zilinifuata kutaka kunisajili, wakiwamo Manchester. Timu ya ajabu ajabu ilinitaka, ni United. Nilizungumza na Van Gaal na hata alileta ofa, lakini hawakuwa timu sahihi kwangu na hakikuwa kipindi mwafaka pia.

"Lakini, sasa nipo kwenye wakati mwafaka, kocha sahihi na klabu sahihi."

Fowadi huyo aliyefunga mabao 20 msimu uliopita alizungumzia pia magumu aliyoyapitia huko utotoni alipokuwa kwao huko Senegal.