Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu za Chikwende kurejeshwa Zimbabwe zatajwa

BENCHI la ufundi la Simba limemrudisha Zimbabwe kiungo mshambiliaji wa timu hiyo, Perfect Chikwende kwa ajili kushiriki michuano ya COSAFA inayotarajiwa kuanza Julai 6 mpaka Julai 18 mwaka huu.

Wakati michuano hiyo ikitarajiwa kuanza stori kubwa ni winga mshambuliaji wa timu ya Simba, Perfect Chikwende kuruhusiwa na uongozi wa Simba kujiunga na timu yake ya Taifa ya Zimbabwe huku Ligi Kuu Tanzania Bara ikiendelea kutimua vumbi.

Chikwende alisajiliwa na Simba Januari 14 mwaka huu katika kipindi cha dirisha dogo la usajili akitokea ndani ya kikosi cha Platinum Fc ya Zimbabwe mara baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika michezo yote miwili ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba.

Baada ya mchezaji huyo kuondoka kocha msaidizi wa Simba Selemani Matola, alisema kuwa lengo la kumruhusu mchezaji huyo  kujiunga na timu ya Taifa ya Zimbabwe ni kumpatia muda mwingi wa kucheza hali itayomfanya kurudisha kiwango chake na kumtengenezea utimamu wa mwili.

Akizungumzia mpango huo kocha msaidizi wa Simba Selemani Matola, alisema kuwa “Ni kweli benchi la ufundi limeamua kumrudisha Chikwende Zimbabwe, kuungana na kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo inayojiandaa na mashindano ya COSAFA, tumefanya hivi kama sehemu ya programu maalum ya kumpa Chikwende muda mwingi zaidi wa kucheza, na kuzidi kuimarisha utimamu wake wa mwili na bila shaka kama atazingatia programu tuliyompa basi atarejea akiwa bora zaidi" alisema Matola.

Mkataba wa Chikwende unamalizika Januari 2022, huku tangu atue Simba amekuwa akipata wakati mkubwa wa kuingia kwenye kikosi cha kwanza na kupelekea kuwepo kwa taarifa kuwa huwenda Klabu hiyo ikafanya maamuzi magumu ya kuachana na kiungo huyo au kumtoa kwa mkopo mwishoni mwa msimu huu.