Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu mechi ya Stars kuchelewa hii hapa

Sababu mechi ya Stars kuchelewa hii hapa

Kumetokea hali ya sintofahamu baada ya mechi ya Taiga Stars dhidi ya Afrika ya Kati kuchelewa kuanza kama ambavyo ilivyopangwa.

Mchezo huo umechelewa kuanza kwa zaidi ya dakika 50 ambapo awali ulitakiwa kuanza majira ya saa 1 :00 usiku kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Taarifa ambazo zimepatikana ni kwamba sababu kubwa ya kuchelewa kuanza kwa mchezo huo ni baadhi ya wachezaji wa Afrika ya Kati kuwa na pasi za kusafiria ambazo sio za mataifa yao.

Ingawa Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Clifford Ndimbo hakuweza kupatikana lakini baada ya dakika 38 timu zote ziliingia tena uwanjani na kupasha tena misuli ingawa tayari walishafanya hivyo mapema.

Mchezo huo hatimaye ulianza majira ya saa 1:50 usiku timu hizo zikicheza mechi yao ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).