Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ruvu, Biashara ngoma bado ngumu

BAADA ya kutoka suluhu kwenye mchezo wa raundi ya 17, Ligi Kuu Bara uliopigwa mchana wa leo Machi 7 kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, Ruvu Shooting na Biashara United zimejikuta zikisalia katika nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoendelea.

Katika mchezo huo, kila timu ilipambana kupata ushindi ili kujikwamua kutoka kwenye nafasi za mwisho lakini ilishindikana na kuifanya Ruvu ibaki nafasi ya 12 na alama 17, huku Biashara ikiishusha mtibwa na kupanda hadi nafasi ya 13 na alama 16 tofauti ikiwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Wakati timu hizo mbili zikishindwa kujikwamua kutoka huko chini, Tanzania Prison, Mbeya Kwanza na Mtibwa Sugar nazo bado hazijaeleweka kwani zipo kwenye nafasi tatu za mwisho kila timu ikiwa imecheza mechi 17.

Katika mchezo wa Ruvu na Biashara, timu zote zilitengeneza nafasi za kufunga lakini zilishindwa kuzimalizia kutokana na washambuliaji wake kutotumia vyema nafasi hiyo.

Ikumbukwe msimu huu, timu mbili za mwisho zitashuka daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitacheza mechi za mtoano 'Play offs' na timu mbili kutoka Championship na washindi watacheza Ligi Kuu msimu ujao.