Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Riyama kaamua mwenyewe tu

Muktasari:

Wapo mashabiki waliorudisha nyuma habari za mwaka jana ambapo tuzo hizo zilidaiwa kuwa na upendeleo baada ya Riyama kukosa Tuzo ya Msanii Bora wa Kike na kupewa Wema Sepetu.

STAA wa filamu za Kibongo, Riyama Ally amewashusha presha mashabiki wake kwa kutoonekana katika Tuzo za Sinema Zetu, zinazoendelea kupigiwa kura na Watanzania.

Huko katika mitandao ya kijamii mashabiki wa Riyama wamechachamaa wakihoji kwanini staa huyo hayumo katika kipengele chochote cha kugombea tuzo wakati mwaka jana alikuwepo.

Wapo mashabiki waliorudisha nyuma habari za mwaka jana ambapo tuzo hizo zilidaiwa kuwa na upendeleo baada ya Riyama kukosa Tuzo ya Msanii Bora wa Kike na kupewa Wema Sepetu.

Hata hivyo, Riyama amezungumza na Mwanaspoti na kutoa sababu ya kwanini hashiriki katika tuzo hizo.

 “Unajua kwa kweli sikupeleka kazi yangu yoyote katika kinyang’anyiro cha tuzo hizo, sababu sina kazi niliyoifanya kwa muda huu. Ila nikijaaliwa mwakani nikifanya kazi nzuri, basi nitapeleka hakuna shida kabisa. Na raha ya kupeleka filamu inapendeza zaidi ukipeleka ya kwako.

“Nawaomba mshabiki wangu, wanielewe hakuna kitu kingine kwani napenda kufanya vitu vya uhakika ili mashabiki wangu waridhike,” alifunguka Riyama.

Hata hivyo, Riyama alisema hakuwahi kulalamikia tuzo za mwaka jana ila watu walishindwa kumwelewa.

“Watu wanashindwa kuelewa kilichotokea tuzo za Sinema Zetu za mwaka jana, sijalalamika kwa kukosa tuzo ila nilikuwa nasema kilichokuwapo.

Riyama alifafanua mwaka huu hakupeleka kazi kwa kuwa hakuwa na taarifa ya tuzo hizo.

 “Binafsi sijaingia kwenye sanaa ili nitumie fursa ya kufanya mambo mengine, bali kuelimisha jamii na kupata kipato kwa kuwa sikusoma lakini nina kipaji.

 “Nimepambana na Watanzania wanajua sasa kwanini watu wanaandaa kitu ili kunivunjia heshima yangu?  Najua ni binadamu waliteleza lakini tunashukuru tumeyamaliza,” alisema Riyama.

Hivi karibuni Kituo cha Azam TV kupitia Chaneli ya Sinema Zetu ilizindua rasmi msimu mpya wa tuzo za kimataifa za Sinema Zetu ambapo washiriki wameshafahamika na kuanza kujinadi katika mitandao kwa kuomba kura kwa Watanzania.

Hata hivyo, Riyama aliliambia Mwanaspoti kioo chake cha jamii ni Msanii,  Monalisa. Maana kabla hajaanza kuigiza alikuwa anamuangalia Monalisa, hivyo ni mwalimu wake na pia ni mkalimani wake.

“Najua watu wengi hawajui, kioo changu cha jamii ni Monalisa, maana kabla sijaanza kuigiza nilikuwa namwangalia na isitoshe ni mwalimu wangu wa Lugha ya Kiingereza,” alisema Riyama mwenye mashabiki wengi kwenye filamu kutokana na uigizaji wake wa maneno Kiswahili.

Akifafanua hilo la maneno ya shombo yenye lahaja za Kiswahili, Riyama  alisema maneno hayo yanatokana na damu yake ya Kizaramo.

“Nashukuru kwa kuwa na mashabiki wengi wanaopenda kazi yangu.

“Wengi hawajui nayatoa wapi maneno yale ya Kiswahili. Kwanza nina damu ya Kizaramo na napenda sana methali za Kiswahili,” alihitimisha.