Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rekodi Simba yaitisha Ihefu SC

Muktasari:

Ihefu SC ilipanda Ligi Kuu kupitia hatua ya mchujo mara baada ya kumalizika kwa msimu wa 2019/2020 ambao ilishika nafasi ya pili katika kundi A la Ligi Daraja la Kwanza.

REKODI iliyowekwa na Simba kwenye Ligi Kuu kwa muda wa miaka mitano (5) inawaweka katika nafasi nzuri kisaikolojia kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa kwanza wa ufunguzi wa Ligi Kuu msimu wa 2019/2020 dhidi ya Ihefu SC utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Jijini Mbeya, Septemba 6 mwaka huu.

Kwa muda mrefu Simba imekuwa na historia nzuri ya kuvuna pointi tatu katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu, iwe katika uwanja wa nyumbani au ugenini.

Tangu ilipolazimishwa sare ya mabao 2-2 katika Uwanja wa Taifa mnamo Septemba 21,2014 katika ufunguzi wa Ligi Kuu msimu wa 2014/2015, Simba haijawahi kudondosha pointi yoyote katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa ligi kwa muda wa miaka mitano, miezi 11 na siku 17 (siku 2178) ikiibuka na ushindi katika mechi zote za namna hiyo katika misimu mitano mfululizo.

Msimu uliofuata baada ya kulazimishwa sare hiyo ya mabao 2-2 na Coastal Union, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi yake ya kwanza kwenye msimu wa 2015/2016 waliyocheza dhidi ya African Lyon.

Nyota hiyo ya Simba kung'aa katika mechi ya kwanza ya Ligi iliendelea katika msimu wa 2016/2017 ambayo waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ndanda mabao yake yakipachikwa na Laudit Mavugo, Fredrick Blagnon na Shiza Kichuya wakati bao pekee la Ndanda likipachikwa na Omary Mponda.

Katika msimu wa 2017/2018, Simba ilianza Ligi kwa ushindi mnono wa mabao 7-0 katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting ambapo mabao yake yalifungwa na Emmanuel  Okwi aliyepachika manne, Juma Liuzio (2) wakati Erasto Nyoni alifunga bao moja.

Ubabe wa Simba uliendelea tena katika msimu wa 2018/2019 ambapo Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Prisons, goli lake likifungwa na Meddie Kagere na msimu uliopita, ikaibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania, yakifungwa na Meddie Kagere aliyepachika mawili na moja likifungwa na Miraji Athuman.

 

Akizungumzia hilo, kocha wa Ihefu, Maka Malwisi alisema kuwa wako tayari kukabiliana na Simba.

"Tulishafahamu mapema kuwa tukishapanda tutakutana na Simba ambaye ni bingwa mtetezi hivyo kiufupi tunaendelea na maandalizi yetu," alisema Malwisi.