Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Refa aliyekataa bao la Aziz Ki kwa Mamelodi, apewa Simba Zenji

REFA Pict

Muktasari:

  • Fainali hiyo imepangwa kuchezwa siku hiyo, baada ya ile ya kwanza itakayofanyika Jumamosi hii huko Berkane, Morocco ikichezeshwa na mwamuzi Pierre Ghislain Atcho kutoka Gabon akisaidiwa na Boris Marlaise Ditsoga (Gabon) na Eric Ayimavo Ayamr Ulrich (Benin), huku refa wa akiba mezani atakuwa Patrice Tanguy Mebiame wa Gabon.

UNAMKUMBUKA yule mwamuzi aliyekataa bao la Stephane Aziz Ki dhidi ya Mamelodi Sundowns lililozua utata mkubwa hadi kwenda kuangaliwa kwenye VAR? Anaitwa Dahane Beida raia wa Mauritania, huyu ndiye ambaye Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limemkabidhi jukumu la kuamua mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mkondo wa pili kati ya Simba dhidi ya RS Berkane ya Morocco itakayopigwa wiki ijayo kwenye Uwanja wa New Amaan, visiwani Zanzibar.

Fainali hiyo imepangwa kuchezwa siku hiyo, baada ya ile ya kwanza itakayofanyika Jumamosi hii huko Berkane, Morocco ikichezeshwa na mwamuzi Pierre Ghislain Atcho kutoka Gabon akisaidiwa na Boris Marlaise Ditsoga (Gabon) na Eric Ayimavo Ayamr Ulrich (Benin), huku refa wa akiba mezani atakuwa Patrice Tanguy Mebiame wa Gabon.

Dahane Beida anakumbukwa kwa tukio la Aprili 5, 2024 lililozua gumzo baada ya shuti la Aziz Ki alilopiga dakika ya 58 dhidi ya Mamelodi Suondowns waliokuwa wenyeji wa mechi ya pili ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Afrika Kusini, kwani licha ya mpira kuonekana kudundia ndani, lakini refa huyo alikataa bao baada ya kwenda kujiridhisha kwenye VAR.

Mechi hiyo ilimalizika kwa matokeo ya 0-0 baada ya awali kushindwa kufunga pia jijini Dar es Salaam na kuamuriwa zipigwe penalti na Yanga ikapoteza kwa mikwaju 3-2.

Rekodi zinaonyesha mwamuzi huyo amechezesha mechi 25 za michuano ya CAF ngazi ya klabu tangu 2019, huku akiwa ameonyesha kadi za njano 97 na nyekundu tatu. Penalti zikiwa saba.

Mwamuzi huyo tayari ameichezesha Simba mechi moja ya African Football League dhidi ya Al Ahly iliyomalizika kwa sare ya 2-2, Oktoba 20, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar, huku akiichezesha Yanga mara mbili, ya kwanza ikiwa ni ile fainali ya mkondo wa pili Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger iliyochezwa Juni 3, 2023 Algeria na Yanga kushinda 1-0. Ya pili ndio iliyokuwa dhidi ya Mamelodi.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Simba kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika tangu michuano hiyo ilipoasisiwa mwaka 2004 kwa kuunganishwa Kombe la Washindi Afrika na lile la CAF ambalo Wekundu hao waliicheza fainali yake na kupoteza 2-0 mbele ya Stella Abidjan ya Ivory Coast.