Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dirisha la usajili lafunguliwa, vita ya vigogo yaanza rasmi

Muktasari:

  • Katika taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilieleza dirisha hilo kubwa litafungwa Septemba 7, 2025, saa 5:59 usiku, huku mchezaji anaweza kuombewa usajili kwa njia tatu kupitia mfumo wa usajili wa FIFA Connnect.

ILE vita ya vigogo vya soka nchini imeanza rasmi baada ya dirisha la usajili la Ligi Kuu, Championship, First League, Ligi Kuu ya vijana chini ya miaka 20 na Ligi Kuu ya Wanawake kufunguliwa  kuanzia Julai 1, 2025 na likitarajiwa kufungwa Septemba 7, 2025.

Katika taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilieleza dirisha hilo kubwa litafungwa Septemba 7, 2025, saa 5:59 usiku, huku mchezaji anaweza kuombewa usajili kwa njia tatu kupitia mfumo wa usajili wa FIFA Connnect.

Njia hizo tatu ni za uhamisho kwa maana mchezaji kutoka klabu moja kwenda nyingine, uhamisho wa mkopo na usajili wa nyota mpya kwenye mfumo.

TFF imezitaka klabu kuambatanisha nyaraka sahihi zilizokamilika zinazotakiwa katika usajili, huku ikiomba atakayekutana na changamoto yoyote katika mfumo huo wa usajili awasiliane na Idara ya Mashindano ya shirikisho hilo kwa msaada zaidi.

Shirikisho hilo limesisitiza, hakutakuwa na muda wa ziada kwa klabu kutokana na tarehe ya dirisha la usajili kufungwa rasmi.

Wakati dirisha hilo likifunguliwa, tumeshuhudia baadhi ya nyota wakitambulishwa na timu mbalimbali huku Simba na Yanga zenyewe zikifanya mambo yao kimya kimya.

 Azam FC imeliamsha mapema kwa kuzinasa saini za aliyekuwa kipa wa kikosi hicho, Aishi Manula kutoka Simba na beki wa kati, Lameck Lawi kutokea Coastal Union.

Nyota mwingine aliyejiunga na kikosi hicho ni kiungo mshambuliaji, Muhsin Malima aliyesajiliwa akitoka, ZED FC ya Misri.

Kwa upande wa sajili nyingine zilizokamilika ni za Namungo FC, iliyowasajili, Cyprian Kipenye kutoka (Songea United) na Abdulaziz Shahame aliyetokea TMA FC ya Arusha, ambapo nyota wote walikuwa wakicheza Ligi ya Championship msimu wa 2024-2025.