Rasmi Simba kuikabili Yanga Kwa Mkapa

Muktasari:
- Nyota huyo anayeongoza wafungaji mabao katika Ligi Kuu Bara akiwa na manane, alisema kuna mambo ambayo hapendi kuyaweka wazi yalitaka kumfanya aondoke.
Simba imethibitisha kucheza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Yanga ‘Kariakoo Derby’ leo d kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mechi hiyo imepangwa kuchezwa kuanzia saa 11:00 jioni ambapo Yanga itakuwa mwenyeji.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Simba imeweka tangazo la mechi hiyo na kuandika ‘Tutakuwepo’.
Uamuzi wa Simba kucheza mechi hiyo leo unatengua taarifa ambayo klabu hiyo iliitoa Juni 12 mwaka huu kwamba haitokuwa tayari kucheza mechi hiyo ikiwa itapangwa tarehe tofauti na 15.06.2025 ambayo awali ndio ilipangwa na Bodi ya Ligi Kuu baada ya mechi hiyo kuahirishwa Juni 8, 2025.
Mchezo huo wa leo una maana kubwa kwa timu zote mbili kwani ndio utatoa uamuzi wa ipi itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kutokana na utofauti wa pointi moja uliopo baina yao kwenye msimamo wa ligi.
Yanga iko juu ikiwa na pointi 79 na inahitaji matokeo ya ushindi au sare tu leo ili iweze kutetea ubingwa ambao utakuwa wa nne mfululizo kwake.
Simba iliyo nafasi ya pili ikiwa na pointi 78, inahitaji ushindi tu ili iweze kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza tangu ilipotwaa kwa mara ya mwisho msimu wa 2020/2021.
Mchezo huo utaamuliwa na mwamuzi Amin Omar atakayekuwa mwamuzi wa kati, akisaidiwa na Mahmoud El Regal, Samir Mohamed wakati mwamuzi wa nne mezani akiwa Ahmed Elghandour wote kutoka Misri huku mtathimini waamuzi akipewa Ali Mohamed kutoka Somalia.
Omar sio mwamuzi rahisi akiwa uwanjani ambapo ana rekodi ya kumwaga kadi nyingi za njano na nyekundu ambapo suala la kuamua penalti sio suala gumu kwake.
Rekodi zake zinaonyesha kuwa amefanikiwa kuchezesha michezo 239, akitoa kadi za njano 823 na nyekundu 20 huku akitoa penalti 85 kwenye michezo yote.