Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia aongeza dau Yanga Sh20 milioni, ila...

Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa Sh20 milioni kwa kila bao la ushindi kwa timu ya Yanga ambayo imetinga fainali za kombe la Shirikisho jana Jumatano Mei 18, 2023.

Katika hatua ya nusu fainali Rais Samia aliahidi kutoa Sh10 milioni kwa kila bao kwa timu hiyo na ilibeba Sh40 milioni ikimfunga Marumo Gallants nje, ndani mabao 4-1.

Rais Samia ametoa ahadi hiyo akizungumza leo katika shughuli iliyoandaliwa na Azam Media ambapo ameweka wazi utaratibu umebadilika na sasa atatoa feda kwa mechi ya ushindi na kuongeza kuwa atatoa ndege kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu msimu huu kwenda Algeria kucheza mechi ya marudiano fainali dhidi ya USM Alger Juni 3 baada ya kuanza kucheza nyumbani uwanja wa Mkapa Mei 28.

"Tunapokwenda kwenye fainali ni Sh20 milioni timu ikitoka na ushindi, hii itatoka na ushindi sio watoke 2-1, ila zaidi ya hapo Serikali itatoa ndege kwenda Algeria,"