PSG wavamia Chelsea

Muktasari:
Manchester United hawana uhakika kama wanaweza kuwa na kipa wao mahiri, David De Gea msimu ujao.Hali hiyo pia ndiyo iliyopo kwenye kikosi cha mabingwa watetezi wa England, Chelsea ambapo kipa wao namba moja Thibaut Courtois huenda akavaa jezi za mabingwa wa Ufaransa, PSG msimu ujao.
Manchester United hawana uhakika kama wanaweza kuwa na kipa wao mahiri, David De Gea msimu ujao.
Hali hiyo pia ndiyo iliyopo kwenye kikosi cha mabingwa watetezi wa England, Chelsea ambapo kipa wao namba moja Thibaut Courtois huenda akavaa jezi za mabingwa wa Ufaransa, PSG msimu ujao.
Habari zinaeleza kwamba, wawakilishi wa Courtois wamekutana na Mkurugenzi wa Ufundi wa PSG, Antero Henrique, kujadili mpango wa kipa huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kutua Ufaransa msimu ujao.