Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Minziro ajitathmini, akiwataja maafande

MINZIRO Pict

Muktasari:

  • Amesema timu hiyo imekuwa na utulivu katika kufanya sajili zake kwani imekuwa ikipata wachezaji sahihi, huku akiipongeza kwa uendeshaji mzuri ambao unaifanya timu kuwa na utulivu na kufanya vizuri.

KOCHA mkongwe nchini, Fred Felix ‘Minziro’ amefanya tathmini yake na kuitaja JKT Tanzania kuwa timu ya mfano na ya kuigwa kwa timu za madaraja ya kati (mid table).

Amesema timu hiyo imekuwa na utulivu katika kufanya sajili zake kwani imekuwa ikipata wachezaji sahihi, huku akiipongeza kwa uendeshaji mzuri ambao unaifanya timu kuwa na utulivu na kufanya vizuri.

JKT Tanzania ni timu pekee katika Ligi Kuu Bara ambayo inaundwa na wachezaji wazawa tu, huku ikinolewa na kocha mzawa, Ahmad Ally. Timu hiyo imemaliza katika nafasi ya sita ikivuna pointi 36 katika michezo 30.

Minziro ambaye ni kocha mkuu wa Pamba Jiji, alitoa kauli hiyo baada ya kufanikiwa kuibakiza timu hiyo kwenye Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao kufuatia sare ya bao 1-1 dhidi ya KMC mwishoni mwa wiki iliyopita.

Pamba imemaliza katika nafasi ya 11 na alama zake 34 baada ya michezo 30, huku ikishinda nane, sare 10 na kupoteza 12, imefunga mabao 22 na kuruhusu 33.

Alisema JKT Tanzania ni miongoni mwa timu ngumu kucheza nazo na siku zote ilimpasua kichwa kufikria namna bora ya kwenda kuwakabili katika mechi walizokutana.

“Hakuna timu katika timu zetu hizi za chini ambayo imefanya usajili bora kama walivyofanya JKT Tanzania, kusema kweli nawapongeza kwa hilo wana timu bora mchezaji ambaye anayeanza na anayetoka wote wako bora,”€ alisema Minziro na kuongeza.

“Nafarijika kwa hilo kuona namna walivyotengeneza timu yao baadhi ya wachezaji nimewahi kuwafundisha leo wamekuwa bora sana.”

Alisema nyakati zote alizokutana na JKT Tanzania alikutana na timu bora kwani haukuwa mchezo rahisi kutokana na ubora wa kikosi chake kwenye eneo la kiungo, mawinga na mabeki wanaofanya kazi kwa ufanisi mkubwa.