Prison waifata Yanga 16 bora FA

Sunday February 28 2021
prison pic
By Ramadhan Elias

KLABU ya Prison imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora baada ya kuifunga Sahare 3-1 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Sheikh Abeid, Arusha leo saa 8:00 mchana.

Ushindi huo unawafanya Prison kukutana na Yanga ambao wao walishinda jana dhidi ya Kengold bao lililofungwa na Fiston Abdulrazack.

Prison ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Adil Buha dakika 10 kisha Gasper Mwaipasi alifunga mara mbili dakika 17 na 28.

Sahare alisawazisha dakika 44 kupitia kwa Dickson Kalinga lakini bao hilo halikuwarejesha mchezoni kwani Prison walionekana kupambana na kulilinda zaidi goli lao.

Mechi nyingine inayochezwa leo ni Coastal Union dhidi ya Ihefu ambayo ilianza kuchezwa saa 10:00 jioni katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Advertisement