Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi Tanzania yajifua Uwanja Uhuru ikijiandaa kuivaa Azam FC kesho

Muktasari:

Polisi Tanzania inajiandaa na mchezo wake dhidi ya Azam Fc utakaochezwa kesho saa kumi jioni.

Dar es Salaam.Kocha mkuu wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini leo asubuhi amewapa darasa wachezaji wake takribani dakika 30 kabla ya kuanza kwa mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kikosi hiko kilifika uwanjani hapa majira ya saa 8:40 asubuhi na iliwachukua dakika tano tu wachezaji kujiandaa na baaada ya hapo walikusanywa na benchi la ufundi na kupelekwa kivulini kuzungumza nao mpaka saa 9:30 Asubuhi.

Katika maongezi yake Malale alikuwa akisadiana na kocha wake msaidizi Ally Mtui aliyeonekana kuweka baadhi ya maneno.

Polisi Tanzania inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Azam Fc utakaopigwa kesho saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Polisi wanaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza 2-0 dhidi ya Coastal Union huku Azam wakiifunga 3-1 KMC.