Pep: Nataka Man United wasahau ubingwa kabisa

London, England. Pep Guardiola ameweka wazi lengo lake akiwa kocha Manchester City ni kuhakikisha anamaliza kabisa utawala wa Manchester United katika soka la England.
Mhispania huyo ametoa kauli hiyo wakati Manchester United ikiwa haijatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England tangu alipostaafu Sir Alex Ferguson mwaka 2013, lakini wamefanikiwa kunyakuwa mataji mengi.
City imefanya uwekezaji mkubwa kuweka tofauti kati yake na majirani zao na hali inavyokwenda wanaonekana wameanza kutawala jiji la Manchester pamoja na soka la England.
Guardiola aliisaidia City kuweka rekodi mpya msimu uliopita, wakitwaa mataji mawili lile la Ligi pamoja na kombe la Carabao, amekiri kuwa anataka kuendelea kubaki na hayo mataji.
“Tuna majirani zetu ambao katika miaka 15 au 20 walizoea kushinda kila wakati. Nafiriki kazi yangu kubwa hapa ni kuhakikisha nabadilisha jambo hilo.”
Guardiola katika msimu wake wa kwanza City alitoka mikono mitupu, lakini msimu 2017-18 alionyesha mabadiliko na kunyakuwa ubingwa.