Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PASI MASTER: Jorginho avunja rekodi ya pasi England

Muktasari:

Kiungo huyo Mtaliano alifanikiwa kutimiza pasi 180 peke yake dhidi ya West Ham

LONDON, ENGLAND. CHELSEA ilipolipa kiasi cha pauni 57 milioni kwenda Napoli kumnunua kiungo wa kimataifa wa Italia, Jorginnho inawezekana watu wengi hawakujua kwamba ilikuwa inamnunua ‘Xavi Hernandez’ mwingine. Anafanya mambo ya hatari na sasa anafunika soka la England kwa pasi.
Juzi katika pambano kati ya Chelsea na West Ham, Jorginho ambaye amechukua uraia wa Italia licha ya kuzaliwa Brazil amevunja rekodi ya pasi katika Ligi Kuu ya England ambayo ilianzishwa katika mfumo mpya mwaka 1992.
Jorginho, 26, alikamilisha asilimia 90 ya pasi zote alizopiga katika pambano hilo la watani wa jadi wa jiji la London. Katika kufanya hivyo alifanikiwa kutimiza pasi 180 kwenda kwa wenzake na kuweka rekodi mpya katika Ligi Kuu ya England.
Awali rekodi ya pasi nyingine katika mechi moja iliwekwa na kiungo wa Manchester City, Ilkay Gundogan katika pambano la upande mmoja dhidi ya Chelsea msimu uliopita. Staa huyo wa Ujerumani alikamilisha pasi 174 na kuweka rekodi.
Kabla ya Gundogan, rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na kiungo mwenzake wa zamani wa Manchester City, Yaya Toure ambaye katika pambano la Ligi Kuu Desemba 2011 dhidi ya Stoke City alifanikiwa kupiga pasi 157 peke yake.
Mwingine aliyekuwa nyuma ya Toure ni nyota wa kimataifa wa Hispania, Santi Cazrola ambaye Mei 2015 katika pambano la Ligi kuu kati ya timu yake ya zamani, Arsenal dhidi ya Sunderland, Cazorla alipiga pasi 154 pungufu ya pasi tatu nyuma ya Toure.
Katika pambano la juzi Jorginho pia aliweka rekodi nyingine kama vile kugusa mpira mara nyingi zaidi ambapo aliugusa mpira mara 191. Jorginho pia aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa pili msimu huu kwa kupiga pasi nyingi katika eneo la adui ambapo alipiga pasi 134.
Tangu msimu wa 2003-04 hakuna mchezaji ambaye alikuwa amejaribu pasi nyingi zaidi katika mechi kuliko yeye. Hata hivyo licha ya utawala huo wa eneo la kiungo kwa Jorginho na wenzake lakini bado walishindwa kuziona nyavu za West Ham na pambano hilo lilimalizika kwa suluhi ya bila kufungana.
Tabia hii ya Jorginho inaanza kumfanya alinganishwe na kiungo wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Xavi Hernandez ambaye anakumbuka kama mmoja kati ya mastaa bora zaidi katika kumiliki mpira na kupiga pasi.
Mwaka 2013 katika pambano la pili la robo fainali Ligi ya mabingwa wa Ulaya dhidi ya PSG, Xavi aliweka rekodi mpya ya michuano hiyo baada ya kumamilisha pasi zake zote kwa asilimia 100 baada ya kupiga pasi 96 ambazo zote ziliwafikia wenzake.
Hata hivyo April mwaka huu katika pambano la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kati ya Real Madrid na Juventus, kiungo wa Madrid, Isco alifanikiwa kuifikia rekodi ya Xavi baada ya kupiga pasi 54 ambazo zote zilifika kwa wenzake. Hata hivyo pasi zake zinabakia kuwa chache kuliko alizopiga Xavi.

Katika michuano ya Euro, Xavi aliwahi kuweka rekodi ya kupiga pasi nyingi zaidi ndani ya mechi moja. Alipiga pasi 859 katika pambano dhidi ya Ireland michuano ya Euro 2012 na hivyo kuweka rekodi katika historia ya michuano hiyo. Katika pambano hilo timu nzima ya Ireland ilipiga pasi 198 ambazo hazikufika walau robo ya pasi alizopiga Xavi.