Parimatch kugawa fursa kwa wateja wake
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe akiwa pamoja na wafanyakazi wa Parimatch
Muktasari:
Kampuni ya michezo ya bahati nasibu Parimatch imeamua kutoa fursa ya kipekee kwa wateja wake wote waliopo ndani ya nchi ya Tanzania, kwa kuwapa fursa ya kijanja ya Uwakala, inayowezesha washiriki wa mchezo wa kubahatihsa kugawiwa kiasi cha hadi asilimia 25% ya faida kampuni inayoipata.
Kampuni ya michezo ya bahati nasibu Parimatch imeamua kutoa fursa ya kipekee kwa wateja wake wote waliopo ndani ya nchi ya Tanzania, kwa kuwapa fursa ya kijanja ya Uwakala, inayowezesha washiriki wa mchezo wa kubahatihsa kugawiwa kiasi cha hadi asilimia 25% ya faida kampuni inayoipata.
Hayo yamebainishwa na Afisa Habari na Mawasiliano Parimatch Tanzania, Ismael Mohamed wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya Sabasaba na kusema kwamba, wamechukua maamuzi hayo kwa lengo la kutaka kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita katika kupambana na utoaji wa fursa kwa vijana pamoja na kugawana kitu kidogo wanachokipata kutoka kwa wateja wao kila uchao.
“Parimatch tumeamua kutoa fursa kwa vijana wa Kitanzania, kwa kutengeneza pesa kiurahisi muda wowote na mahali popote kwa kuwa wakala wetu. Inawezekana kutumia Muda wako wa Ziada kujiongezea kipato. Njoeni huku mjitajirishe vijana, mshike mkono rafiki yako ili mtoke kimaisha kwa pamoja”,alisema Mohamed.
Aidha, Mohamed alisema kuwa Parimatch inajivunia kuanzisha vitu yenye utofauti wa hali ya juu ukilinganisha na makampuni mengine sokoni.
“Program yetu ina tofauti kubwa na makampuni mengine inavyoendesha, sisi tupo katika hali ya kuwasaidia vijana nasio kuwa kandamiza, na ndio maana kwetu hakuna ada ya kujiunga, malipo yapo kwa wakati, mawasiliano yetu ni moja kwa moja kupitia kitengo chetu cha huduma kwa wateja saa 24 siku 7 za wiki. Pia sisi hatulipi mawakala kwa target ya wateja bali sisi tunalipa kila baada ya muda wa wiki mbili kile ambacho wakala amevuna kupitia wateja wake na mawakala aliowasajili kupitia promo code yake”, alisisitizia Mohamed.
Mbali na hilo, Mohamed alisema kuwa Parimatch tokea iingie sokoni imeweza kubadirisha hali ya soko ya zamani ya kubashiri kutoka kwenye kamari hadi kuwa burudani ambapo kila kijana aliyevuka miaka 18 huburudika kwa kubeti na Parimatch ambayo inaongoza hadi sasa kwa kuwa na masoko mengi ya uchaguzi kwa kila mechi.
Parimatch ndio kampuni namba 1 inayowawezesha wateja wake kutochana mkeka kwa kutumia Cashout ambayo ina mruhusu mteja, kunusuru pesa iliyowekwa isipotee na mechi zilizoharibika kwenye mkeka mmoja.